Thursday, July 07, 2016

MILION 13 ZAPATIKANA KUFANIKISHA VYOMBO VYA INJILI VINGUNGUTI:

Na Unique Maringo
Mchungaji kiongozi Moses Mapunda  wa kanisa la International Evangelism,lililoko Vingunguti jijini Dar es salaam,kwa kushirikiana na watende kazi wa kanisa hilO Wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shingi milion kumi na tatu laki tano  kati ya milioni kumi natano zilizo kuwa zinahitajika lengo likiwa ni  kufanikisha ununuzi wa wavyombo vya Injili.

Katika harambee  hiyo ambayo iliongozwa  na mgeni wa heshima ndugu Deogratius Senya, ambaye alitoa keshi shilingi Milion moja na laki mbili, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa CPCT Ilala na watumishi wa Mungu mbali mbali,nakufanikiwa  kukusanya fedha hizo zenye lengo la kununua vyombo vya Injili ili kuharibu makazi ya vikundi vya uhalifu vilivyo piga kambi katika  maeneo ya vingunguti Ilala jijini Dar es Salaa.

Ili kufikia  malengo la kukusanya Milioni  kumi natano , Ndugu Senya aligawa saa za ukutani kumi na mbili,kwa watu kumi na mbili wa kwanza walio muunga mkono,ambapo saa moja yenye thamani ya shilingi elfu hamsini,ilitoa shilingi laki mbili.

Katika harambee hiyo Sanya alisema kuwa kutokana na watoto wengi kuishi katika mazingira ya uovu ni jukumu lakila mkristo au mtanzania mwenye mapenzi mema na watanzania wenzake kusaidiana kuwatoa vijana na watoto walio jiingiza katika uvutaji wa madawa ya kulevya pamoja na ujambazi, ubakaji jambo ambalo lina letea fedhea wazazi wengi na kujikuta katika magonjwa ya shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.

 "Mna jua kama hatuta kubali kushirikiana na mchungaji Moses kuhubiri Injili ili kuwanusuru vijanana ambao wamesha aribikiwa kuna siku watawafundisha watoto wako kujiingiza katika vitendo viovu,hivyo toa fedha yako ili tusaidiane kukata huu matandao wa uhalifu ambao umesababisha familia nyingi kuwa na vilio visivyo koma kutokana na watoto kujiingiza katika uhalifu na kupoteza hatima yao.

Kila mzazi anamtegemea mtoto wake ndio maana tunawasomesha na kuwajengea mazingira mazuri lakini endapo sisi wenyewe hatutajali basi jua kama sio mtoto wako kukumbwa na uonevu huu wa adui kunasiku mjukuu wako atajikuta mikononi mwa kundi hili,dawa ni kuwahubiria Injili ili kuvunja mtandao wao kwakua watakuja kwa Yesu na watakua watu wazuri".alisema Sanya

Kwa upandea wake Mchungaji Moses alisema kuwa kutokana na eneo lake la vingunguti kukabiliwa na vijana wengi wanaojihusisha na vitendo viovu ambavyo ni tishio kwa wanachi wa eneo la vingunguti na maeneo ya jirani,ameamua kuangana na Jeshi la Polisi nchini kuhamasisha wananchi utii wa sheria bila shurti kwa kuamua kuwahubira Neno la Mungu ili waweze kuishi maisha yanayo mpendeza Mungu na wanadamu.

 Vijana na watoto wamekuwa  wezi,wabakaji na wavutaji wa dawa za kulevya kutokana na kuwa katika vifungo vya kipepo hivyo hata jeshi la Polisi wakiamua kuwakamata na kuwafunga gerezani,wakiachiliwa watakua hivyo hivyo hawata badilika kwa kua kila jambo analo lifanya mtu ambalo ni chukizo kwa Mungu nyuma kunaroho chafu inayo mhimiza kufanya vitendo hivyo.

Aliongeza kutokana na fumbo hilo ambalo limefumba vijana na baadhi ya viongozi wa siasa na wazazi ambao hawajui hatima ya watoto wao ameadhimia kufanya mikutanao ya Injili kwa kushirikiana na watumishi wa Mungu mbali mbali ili kuhakikisha wanawafikia vijana hao ambao wako katika vifungo vya kipepo.

Aidha kutokana na uwepo wa vikundi vya ualifu katika maeneo ya vingunguti,Mchungaji Moses alisema kuwa kikundi ambacho ni tishio kwa wanachi ni kundi linalo jiita 'Frimason Camp'.alisema vijana hao wako zaidi ya thelathini hubaka watu hadhara mchana na kuwapora vitu walivyo navyo pasipo uoga wowote.

Alisema licha ya Jeshi la Polisi kupambana na vijana hao na kuangamiza kituo hicho  lakini kila kukicha kundi hilo huongezeka vijana kutoka maeneo mbali mbali,jambao ambalo limemsababisha Mch,Moses kuamua kuhubiri Injili kwa kufanya mikutano ya nje pamoja na maombezi kila vijana hao walipoweka kituo.

Kwa upande wa vibali vya Mikutano ya nje alisema kuwa anavyo vibali tayari ambayo walipewa na Mwenyekiti wa CPCT Mkoa wa Dar es Salaam,Dkta Bruno Mwakibolwa,hivyo vyombo hivyo vya Ijili kazi yake ni kuvunja vikundi hivyo vya ualifu vingunguti.

No comments:

Post a Comment