1-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea wakati wa hafla ya utoaji madawati kwa waheshimiwa wabunge kwa ajili ya shule zilizo kwenye majimbo yao ambapo pamoja na kuishukuru ofisi ya Bunge kwa kazi hiyo pia ameahidi serikali yake kuendelea kukabiliana na changamoto zilizokatika sekta ya elimu ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na mazingira rafiki ya kujifunzia. Katika viwanja vya Karemjee Jijini Dar es Salaam.
