Na : Mwandishi Wetu
Mamalaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imewashauri wananchi na Mamlaka za Miji kuhakikisha kuwa mifumo na njia za kupitisha maji katika maeneo yao inafanyakazi kwa kiwango cha kutosha ili kuepuka madhara yanayowezo kutokana na mvua za msimu zinazotarajiwa kuanza Mwezi Machi.