Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimsikiliza Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Michael Baror alipotembelea Taasisi hiyo jana kwaajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya Moyo wanazozitoa. Mhe. Naibu Balozi Baror aliahidi nchi yake kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo ili watanzania waendelee kupata huduma bora za matibabu ya Moyo. Mwanzoni mwa mwezi ujao jumla ya watoto tisa wanatarajia kwenda nchini Israel kwaajili ya matibabu ya moyo.
