Showing posts with label Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Show all posts
Showing posts with label Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Show all posts

Friday, February 17, 2017

WATUMISHI WAWILI WA TRA WANASHIKILIWA NA VYOMBO VYA DOLA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA

Watumishi Wawili Wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanashikiliwa na vyombo vya dola wakituhumiwa kujihusisha na upitishaji Wa kemikali ambazo hutumika kutengenezea dawa za kulevya aina ya Heroin.

Kukamatwa kwa watumishi hao wa umma kumetangazwa na Kamishina Wa Operasheni ya Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya Mihayo Msekela.
Kamishina wa Oparesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na kupambana na dawa za kulevya,Mihayo Msikhela akifafanua japo alipokuwa akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mapema leo,katika ofisi za Mamlaka hizo zilizopo Upanga,jijini Dar Es salaam kuhusiana na Operesheni za kuwakamata watuhumiwa waliojihusisha na biashara haramu ya usafirisha wa dawa za kulevya hapa nchini,ambapo katika Oparesheni hizo zinazoendelea nchini,ilionesha mafanikio kwa baadhi ya mikoa kama taarifa inavyoonesha hapo chini.PICHA NA MICHUZI JR.

Thursday, August 11, 2016

MAHAKAMA KUU YATENGUA HUKUMU YA AWALI YA KUWAFUTIA SHTAKA LA UTAKATISHAJI FEDHA ALIYEKUWA KAMISHNA MKUU WA TRA NA WENZAKE


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua uamuzi uliotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Emmilius Mchauru wa kufuta shtaka la kutakatisha Dola Milioni 6 za Kimarekani baada ya kuona liliondolewa kinyume cha sheria!

Kesi hiyo inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) (pichani kati) Harry Kitilya na wenzake dhidi ya mashtaka manane ikiwamo la kutakatisha fedha na walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Aprili Mosi Mwaka huu. 

Friday, July 08, 2016

SERIKALI YAFUNGUA OFISI ZA NIMROD MKONO

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jana imezifungua ofisi za Kampuni maarufu ya uwakili ya Mbunge wa Butiama, Nimrod Mkono, ikiwa ni siku chache baada ya kuzifungia kwa madai kuwa kampuni hiyo inadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.