wa Simanjiro, Mheshimiwa James Ole Millya ametoa pongezi kwa viongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa jinsi wanavyojali na kuwahudumia wananchi.
Ametoa pongezi hizo jana (Alhamisi, Februari 16, 2017) kwenye mikutano miwili ya hadhara iliyofanyika Orkesumet na Mererani wilayani Simanjiro, Manyara, baada ya kupewa nafasi asalimie wananchi kabla Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hajazungumza na wakazi wa maeneo hayo.