Saturday, April 30, 2016

KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI CHAFUNGUA MAFUNZO YA KUPUNGUZA AJALI,VIFO NA MAJERUHI BARABARANI

Mwenyekiti wa kamati ya Bloomberg Initiative Global Road Safety Tanzania,Mrakibu Msaidizi wa Polisi Mathew Msuyale akimkaribisha mgeni rasmi(hayupo pichani)pamoja na wadau wa mafunzo hayo.

CCM MWANGA WAJIVUNIA KUTOVURUGWA NA WAPINZANI

Kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anapanda mti nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Mwanga

UCHUKUZI SC VINARA MEI MOSI WATWAA VIKOMBE 11

Mwanaisha Athuman wa Uchukuzi SC akipokea kombe la ubingwa wa netiboli kutoka kwa mgeni rasmi Mwenyekiti TRAWU, Mussa Kalala, katika mashindano ya Mei Mosi.

MBATIA AMUONGOZA MKURUGENZI WA IDARA YA MAAFA NCHINI KUTEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA KWA MAFURIKO

Madereva wa bodaboda wakijaribu kupita katika eneo hilo kwa umakini mkubwa. 
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko.

MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA AZINDUA KAMPENI YA USAFI JIJI LA DAR:

;

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda (wa pili kushoto),akiwa sambamba na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa za Wilaya ya Kinondoni,Ilala pamoja na Temeke wakishiriki kwa pamoja kufagia ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono Mh Paul Makonda kuzindua kampeni ya Usafi wa jiji la Dar Es Salaam,uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika mapema leo asubuhi Katika viwanja vya .Lidaz Club,Kinondoni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali serikali,dini na makundi mengine yakiwemo makundi ya michezo na waendesha boda boda.Mkuu wa Mkoa alizindua kampeni hiyo ya Usafi kwa kuwakabidhi Wenyeviti hao kila mmoja ufagio wa ajili ya kwenda kuwahamasisha wananchi wao katika mitaa yao.

Friday, April 29, 2016

TIMU ZA MPIRA WA PETE NA MIGUU ZA BUNGE ZAPONGEZWA KWA KUFANYA VIZURI MASHINDANO YA MUUNGANO.

Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Akson akitoa maelekezo wakati wa mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AWASILI MKOANI DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma wakati akitokea mjini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.

MADIWANI WILAYA YA HAI WAIKACHA KIKAO CHA MKUU WA MKOA:

Mkuu wa mkoa wa kilimanjaro mhe.Said Meck Sadiki akizungumza katika kikao.
Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza katika kikao hicho.

CHANJO YATOLEWA KWA WATOTO CHINI UUA MIAKA MITANO KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO:

Na Magreth Kinabo- Maelezo

Jamii imeshauriwa  kuwapeleka watoto wote wanaostahili kupata chanjo    walio chini ya umri wa miaka mitano katika vituo vya afya ili waweze kupatiwa chanjo  ili kuweza kutokomeza maradhi na kupunguza vifo vya watoto.
Kauli hiyo ilitolewa Aprili 27, mwaka huu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Mpoki Ulisubisye wakati wa maadhimisho ya wiki ya chanjo nchini yaliyofanyika  kwenye hoteli ya Serena Jijini Dares Salaam.
Alisema  utoaji wa chanjo hiyo umeaanza Aprili 25 hadi 29 mwaka huu na  kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘ Kumilisha Chanjo,Epuka Ugonjwa wa Polio’. Hivyo  vituo  vya  kutolea huduma za afya vinafunguliwa kuanzia saa 2: 00  asubuhi hadi saa 11.00 jioni.
“ Kila mmoja wetu anawajibu wa kuhakikisha  mtoto wake , mtoto wajirani au mlengwa mwingine yeyote anapewa haki ya chanjo ili kumzuia asipatwe na maradhi ambayo yanakingwa na chanjo au asiwe na hatari kwa wengine kwa kuwaletea ugonjwa,” alisema Dkt. Ulisubisye.

TRUMP ACHEMKA KUTAJA JINA LA TANZANIA:

Trump

Image copyrightAP
Image captionTrump alishambulia sana sera ya kigeni ya Obama
Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump amekejeliwa mtandaoni baada ya kuonekana akiboronga akitamka Tanzania wakati wa kutoa hotuba.
Bw Trump alikuwa akizungumzia mashambulio ya kigaidi yaliyotekelezwa katika mabalozi ya Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 wakati wa kuzungumzia sera yake ya kigeni.
Badala ya kutamka vyema ‘Tanzania’ anasikika akitamka ‘Tan-zay-nia’.
Mashambulio hayo yalitekelezwa na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda.
Msemaji wa ikulu ya White House pia alimcheka Bw Trump alipoulizwa kuhusu vile mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York alivyotamka jina Tanzania.
“Kweli, yamkini jinsi ya kutamka huwa haijaelezwa kwenye kifaa cha kuonesha maandishi ya hotuba,” alieleza afisa wa habari wa ikulu Bw Josh Earnest.
Wakati wa hotuba hiyo, alizungumzia pia kuhusu kundi la Islamic State ambalo kwa sasa limeanza kunawiri nchini Libya. Kundi hilo hujulikana pia kama Isis.
“Na sasa Isis wanapata mamilioni na mamilioni ya dola kila wiki kwa kuuza mafuta ya Libya. Na wajua? Huwa hatuwawekei vikwazo vya kutouza, hatuwaangushiwi mabomu, hatufanyi lolote,” alisema.
“Ni kana kwamba nchi yetu haifahamu yanayofanyika, jambo ambalo huenda likawa kweli.”
Kwenye hotuba yake, Bw Trump alikosoa sera za kigeni za Rais Barack Obama.
Lakini Bw Earnest alipuuzilia mbali madai ya Bw Trump ambaye kwa sasa anaongoza miongoni mwa wagombea wanaotaka kupeperusha bendera ya chama cha Republican.

JUHUDI ZA KUTOKOMEZA UGONJWA WA MALARIA DUNIANI:

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Kufanikiwa kwa juhudi za Kutokomeza ugonjwa wa Malaria kutaufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri na salama pa kuishi kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo na kuwawezesha mamilioni ya watu kufikia malengo yao kimaisha.

Hivi karibuni Tanzania imeungana na nchi nyingine Ulimwenguni kuadhimisha siku ya Malaria duniani ambapo ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo katika jamii.

Takwimu kutoka Shirika la Afya ulimwenguni WHO za mwaka 2002 zinaonyesha kuwa kila mwaka watu kati ya milioni 300 hadi 500 duniani wanapata ugonjwa wa malaria, kati yao watu milioni moja na nusu hufariki kutokana na ugonjwa huo.

Kulingana na takwimu hizo katika bara la Afrika watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano ndiyo wanaathirika zaidi na ugonjwa wa malaria ambapo kila mwaka watoto milioni tano wanakufa kwa ugonjwa huo barani Afrika.

Kwa mujibu wa WHO idadi  vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria hadi kufikia mwaka 2013 vilipungua kwa takriban asilimia 20 tu duniani kote katika muongo mmoja uliopita ambapo theluthi moja ya nchi 108 ambazo malaria ilikuwa imeenea zilitarajiwa kutokomeza ugonjwa huo katika kipindi cha miaka 10.

Utekelezaji Wa Sera Ya Miundombinu

DC WA KINONDONI ALLY HAPI AANZA MAPAMBANO DHIDI YA WATUMISHI HEWA, ABAINI 89 WALIOLIPWA ZADI YA SH BILIONI 1.331


Mkuu  wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema idadi ya watumishi hewa katika wilaya hiyo, imeongezeka hadi kufikia 89 wakiwa wamesababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni moja.

Aidha, Hapi amebaini uwepo wa watumishi vivuli 81 katika kada ya ualimu na hivyo kutoa siku saba kwa maofisa utumishi wa wilaya hiyo, kuhakiki watumishi vivuli ili kubaini idadi yao na hasara waliyosababisha.

Hapi aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, na kueleza kuwa awali wakati akiingia katika ofisi yake wiki iliyopita alikuta kuna watumishi hewa 34 waliokuwa wamesababisha hasara ya Sh milioni 512.

Alisema baada ya kufanya uhakiki zaidi walibainika watumishi hewa wengine 55 walioisababishia serikali hasara ya Sh milioni 619 na hivyo kufanya jumla ya hasara kuwa Sh 1,131,754,081.

“Bado uhakiki wa kina unaendelea ili kuhakikisha tunamaliza hili tatizo la watumishi hewa katika wilaya ya Kinondoni, awali walikuwa 34 lakini sasa wameongezeka 55 na kufikia 89,” alisema Hapi.

Akifafanua kuhusu watumishi vivuli, Hapi alisema watumishi hao ni wale ambao walihamishwa bila kufuata taratibu na hivyo kuendelea kupokea mshahara wa kazi yake ya awali badala ya kazi yake mpya.

Alisema walibaini kuwepo kwa walimu katika idara ya elimu ya msingi 42 ambao baada ya kufuatilia hawakuonekana katika shule yoyote ya wilaya hiyo.

“Kwa hiyo hili nalo ni tatizo kuna walimu wengine wanapokea mshahara mkubwa, lakini mtu alishahamishwa lakini anaendelea kupokea mshahara wa zamani ambao haufanyii kazi,” alisema.

Katika hatua nyingine, Hapi aliwataka wafanyabiashara ndogo ndogo walioko katika maeneo yasiyoruhusiwa kuondoka katika maeneo yasiyoruhusiwa baada ya siku saba alizotoa kukamilika.

Alisema agizo hilo alilitoa ikiwa ni sehemu ya kuweka Manispaa ya Kinondoni katika hali ya usafi ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya Rais John Magufuli ya usafi wa kudumu.

SERIKALI KUWASILISHA MSWADA WA SHERIA YA NDOA:


Serikali   imejiandaa kuleta Muswada wa Sheria bungeni kutoa haki ya kusoma kwa watoto wote wa kike na kiume wa shule za msingi, sekondari na kutoruhusiwa kuoa au kuolewa.

MAFURIKO MAKUBWA DAR ES SALAAM NA NAIROBI KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

Image captionMadhara ya mvua kubwa mjini Dar es Salaam
Hali ikuwa tete na ikawa  siku ngumu sana kwa uchukuzi mjini Dar es Salaam, 
Kisa na maana,,,,mafuriko.



Pamoja na jitihada za Serikali kuhamasisha Wananchi kutoka katika maeneo Hatarishi Mabondeni, ambayo kwa kipindi cha mvua huathirika zaidi. Wananchi wa baadhi ya Maeneo ya Mabondeni, hususani eneo la Mto Msimbazi wamepatwa na adha kubwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam.Katika picha ni baadhi tu ya maeneo yaliyoathirika.Athari hizo zimeonekana katika maeneo mbalimbali kama vile Jangwani,Mbezi Beach,Tandale kwa Tumbo.


Image captionWenyeji walitatizikika kuendesha shughuli zao za kawaida
Baadhi ya barabara kuu za kitovu hicho cha kibiashara cha Tanzania, zilikuwa hazipitiki.
Image captionMaji kila mahali
Mvua kubwa inayoendelea kunyesha hivi sasa kanda yote ya Afrika Mashariki imesababisha mafuriko makubwa ambayo muundo msingi wa barabara za miji ya Nairobi na Dar es Salaam haziwezi kumudu.
Magari ambayo yalijaribu kutumia mabarabara ya Dar es Salaam yalikwama mengine huku yale yenye kimo cha juu yakifaulu kupita.
Image captionMagari mengi yamekwama barabarani
Wenyeji sasa wameanza kuhoji uwezo wa muundo msingi wa maji taka wa mji huo wa Dar es Salaam hususan ukizingatia kuwa ndio sasa msimu wa mvua umeanza.
Mtangazaji wetu wa Dar es Salaam Sammy Awami amefaulu kuondoka nyumbani kwake na katika pita pita zake ametutumia picha hizi zinazoonesha hali halisia ya baadhi ya mabarabara ya Dar es Salaam.
Image captionWenye magari mjini Nairobi wataabika mabarabarani
Nchini Kenya hali sio tofauti.
Barabara ya kisasa ya Thika Super Highway haipitiki baada ya mvuo kubwa kunyesha mchana na kusababisha mafuriko makubwa.
Image captionMtabiri wa hali ya hewa anasema mvua bado inatarajiwa
Kinaya ni kuwa mtabiri wa hali ya hewa anasema kuwa mvua kubwa inatarajiwa kunyesa mjini Nairobi na maeneo mengi ya nchi.
Wenyeji wa mji huo wa Nairobi wameanza kutoa hasira zao kwenye mitandao ya kijamii wengi wakipiga picha maeneo yaliyokumbwa na mafuriko.

MTOTO WA MIAKA MIWILI AMUUA MAMA YAKE KWA RISASI HUKO MAREKANI:

Price

Image copyrightAP
Image captionPrice alipigwa risasi na mwanawe akiendesha gari
Mvulana wa umri wa miaka miwili amempiga risasi na kumuua mamake kimakosa katika mji wa Milwaukee, Marekani.
Mtoto huyo alipata bunduki hiyo sehemu ya nyuma ya gari.
Mwanamke huyo, Patrice Price, 26, alikuwa akiendesha gari la mpenzi wake ambaye ni mlinzi na ambaye alikuwa ameacha bunduki yake kwenye gari, babake Andre Price amesema.

Thursday, April 28, 2016

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MTENDAJI TIC


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bi. Juliet Kairuki kuanzia tarehe 24 Aprili mwaka huu.

WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAUWAWA MKOANI MBEYA:

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya (Hawapo pichani)katika kuzngumzia tukio la kuuwawa kwa majambazi watatu wakati wakijaribu kufanya uhalifu katika duka la kuuzia vinywaji mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Butusyo Mwambelo akionyesha silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine ambayo ilikuwa ikitumika na majambazi hao katika tukio la kutaka kufanya uhalifu kwenye duka la vinywaji mali ya Hamisi mji mdogo wa Matundasi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya April 27 mwaka huu.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KWA RAIS VLADMIR PUTIN WA URUSI NA KUFUNGUA MKUTANO WA MAMBO YA FEDHA KWA WANAWAKE:

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia unga unaotokana na matunda ya mashelisheli pamoja na bidhaa mbalimbali za matumizi ya Nyumbani zinazofanywa na wajasiriamali wadogowadogo alipotembelea maonesho baada ya kufungua mkutano unaojadili kuhusu  mambo ya kifedha unaoangalia jinsi Mwanamke atakavyoweza kuingia kwenye mifumo yote ya kiuchumi hasa katika upatikanaji wa mikopo na mitaji kwa Mwanamke utakaorahisisha kufanya kazi zao kwa ufanisi. Mkutano huo umefunguliwa April 28,2016 katika Ukumbi wa BOT Dar es salaam.(Picha na OMR) 

RC.MAKONDA AWATAKA WAMILIKI WA KUMBI ZA STAREHE PAMOJA NA WAMILIKI WA BENDI KUPELELEKA MAPENDEKEZO MAPYA SHERIA YA KUFANYA BIASHARA HIYO.

Sehemu ya wamiliki wa Kumbi za Starehe,Bendi na Wanamuziki wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam. 

ELIMU YA UZAZI WA MPANGO YATOLEWA KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA ITOBO SIMIYU

Mtaalam wa masuala ya uzazi wa mpango kutoka Marie Stopes Tanzania, Bi. Ester Meena akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu mapema wiki iliyopita. Elimu hiyo ya uzazi wa mpango iliendana na huduma ya upimaji wa afya ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya uzazi wa mpango. Wananchi wa kijiji cha Itobo, Itirima - Simiyu wakipatiwa elimu ya uzazi wa mpango.

Wednesday, April 27, 2016

SERIKALI YAKIRI UPUNGUFU WA SUKARI, YAAGIZA NJE YA NCHI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza maofisa biashara wa wilaya, mikoa na Taifa kukagua maghala yote ya wafanyabiashara walioficha sukari na kuwachukulia hatua.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 10 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA 10 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Ndugu Jumanne Abdallah Sagini kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

USAID WAZINDUA MRADI WA UIMARISHAJI MIFUMO YA SEKTA ZA UMMA MKOANI MTWARA:

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu akitoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa Uzinduzi wa kimkoa wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma, unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MAAFISA WATEULE DARAJA LA KWANZA , MKOANI MOROGORO


 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja katika jukwaa akipokea salaam ya heshima kutoka Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).

KIJIJI CHA NYEBURU CHAPATA MKOMBOZI WA MRADI WA UMEME WA VIJIJINIKIJIJI CHA NYEBURU CHAPATA MKOMBOZI WA MRADI WA UMEME WA VIJIJINI

Pic 17NA VICTOR MASANGU,
WAKAZI zaidi wa 100 katika kijiji cha Nyeburu Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani waliokuwa na tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme na kuishi katika giza kwa kipindi cha muda mrefu kwa sasa wamenufaika baada ya kuunganishiwa umeme kutokana na kukamilika kwa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu wa pili.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA UONGOZI WA BARAZA LA TAWLA NA UONGOZI WA SKAUT LEOMAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA UONGOZI WA BARAZA LA TAWLA NA UONGOZI WA SKAUT

mak1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na uongozi wa Baraza la Wanachama waChama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam April 27,2016  kwa lengo la kumpongeza na pamoja na kumuelezea malengo na mikakati ya kiutendaji ya Chama hicho.