Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na mali zilizopo jiji la Dar es Salaam kuwa zipo chini ya jiji la Dar es Salaam. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Saed Kubenea akionyesha baadhi ya nyaraka za siri za jiji la Dar es Salaam ambazo wameanza kuzichambua kwaajili za kutambua mali zilizo chini ya jiji la Dar es Salaam. katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita na Afisa habari wa Ukawa, Gasto Makwembe.
Kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kuanza kuchunguza mali za jiji la Dar es Salaam, (Katikati) Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Halima Mdee na Kulia ni Mjumbe wa baraza la jiji la Dar es Salam, Saed Kubenea wakiwa katika mkutano wa Meya wa jiji la Dar es Salaam.
BARAZA la Madiwani la Jiji la Dar es Salaam limeunda kamati ya kuchunguza mali za jiji hilo kutokana na mali hizo kugubikwa na mbinu chafu na jiji kushindwa kunufaika mali hizo.
Akizungumza leo na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema kuwa kamati hiyo lazima ichambue mali hizo na kama ziko kwenye mikataba nazo ziangaliwe jinsi walivyoingia.
Amesema kuwa katika mali hizo ni pamoja na vibanda 130 vilivyo katika Benjamin Mkapa Kariakoo waliopanga vibanda hivyo wanalipa sh.30,000 ambapo kwa kiwango hicho ni kidogo sana kutokana eneo vilipo.
Mwita amesema kuwa mali za jiji zimekuwa hazinufaishi na kufanya mapato kukusanywa sh.bilioni 11.7 hivyo mali zote zikichambuliwa jiji linaweza kukusanya zaidi ya sh.bilioni 20.
Aidha amesema kuwa UDA ni mali ya jiji kutokana na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuzungumza kuwa shirika la Uda ni mali ya jiji.
Mwita amesema vyanzo vingine ambavyo jiji haipati fedha ni Soko la Kariakoo, DDC hivyo vikiamgaliwa na kamati iliyoundwa itaonyesha hali halisi na jinsi jiji watavyonufaika.
No comments:
Post a Comment