Saturday, April 16, 2016

MWANAFUNZI MTANZANIA ASHIRIKI ONYESHO LA UBUNIFU LILILOANDALIWA NA RAIS BARACK OBAMA

 .Oh "Kumbe kinafanya kazi hivi" ndivyo anavyoelekea kusema Rais Obama mara baada ya kuweza kukiendesha kifaa hicho kwa kutumia simu, aliyechuchuma ni Stephen Mwingira ambaye pamoja na Wendy Ni na Armon Halwan walipata fursa ya kuonyesha ubunifu wao katika onyesho la mwisho  lililoandaliwa na Rais  Barack Obana na kufanyika White House  April 13. 2016.
 .Mwanafunzi  Armo Halwan akimuelekeza Rais  wa  Marekani,Barack Obama anavyoweza kutumia simu  kuendesha   cha  kufanyia usafi ( Vacuum Cleaner) kilichobuniwa na wanafunzi wa Baruch Collage Campus High School ya Jijini New York kupitia timu yao ya  ufumbuzi (Invent Teams)katikati ni Wendy Ni na anayefuatia ni  Stephen Mwingira ( mtanzania) anaonyesha  namna gani  kifaa hicho kinavyofanya usafi kwenye njia za treni za ardhini ( Subways).
 Stephen  Mwingira na Wendy Ni, wakiangalia kwa makini  jinsi Rais Obama anavyoelekezwa namna ya kutumia simu  kuendesha  mashine hiyo katika Onyesho la ubunifu wa kisayansi ambalo lilifadhiliwa na Rais Barack Obama katika Ikulu ya  Rais ( White House Science Fair 2016)
  Rais Barack Obama akipeana  mkono na Stephen  Mwingira na timu yake baada ya kumaliza kutoa maelezo yao kifaa walichokibuni. Kwa miaka sita Rais Barack Obama amekuwa akifadhili  maonyesho ya ubunifu wa   vifaa mbalimbali   vilivyobuniwa na wanafunzi kuanzia wale wa shule za wali  hadi  sekondari ikiwa ni jitihada zake za kuwahamasisha wanafunzi  kupenda masomo  ya sayansi, teknolojia na hesabu tangu wakiwa wadogo na hivyo kuibua vipaji vyao. katika onyesho hilo la mwisho wa utawala wa Barack Obama jumla ya wanafunzi 130 kutoka states mbalimbali walishiriki.

Stephen Mwingira akiendelea kutoa maelezo zaidi  kwa Rais Obama namna kifanya cha kufanyia  usafi  kwenye njia za reli ambacho ni cha gharama nafuu kinavyofanya kazi.


 April 13, 2016,  Rais wa Marekani, Barack Obama, alifadhili  onyesho  la mwisho  katika utawala wake,  onyesho lililohusu ubunifu katika Nyanja za  sayansi ambalo  limewahusisha wanafunzi  kuanzia shule za  awali,msingi hadi za sekondari  kutoka  States  mbalimbali za  Marekani.

Kwa miaka sita tangu mwaka 2010, Kiongozi huyo wa Marekani amekuwa akifadhili onyesho hilo  lijulikanalo  kama White House Science Fair  ambalo limekuwa  likifanyia  katika  Ikulu yake  (White House) lengo likiwa ni  kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi,  hisabati ,teknolojia  na  ufundi ( STEM)na hivyo   kuibua  vipaji  vya  ubunifu   mwiongoni  mwa wanafunzi ( young inventors) . 

Katika onyesho hilo la  Aprili 13  jumla ya wanafunzi 130  walishiriki baada ya kukidhi vigezo vya kuingia katika  onyesho hilo. Miongoni mwa wanafunzi  waliopata fursa hiyo adhimu ya  kushiriki  baada ya kukidhi vigezo ya  ubunifu wao ni    mwanafunzi mtanzania  Stephen Wilfred Mwingira ambaye pamoja na wenzake wawili Armo Halwah na Wendy Ni  wanaosoma  Baruch College  Campus High School ya jijini New York,  wamebuni kifaa cha gharama nafuu ( vacuum  cleaner)   kinachoweza kutumika katika  kusafisha   njia za reli   za chini ya ardhi ( Subways). 

Stephen Mwingira na timu yake,  walipata fursa ya  kuelezea  na  kuonyesha mbele ya Rais Obama namna gani kifaa walichobuni  ( Vacuum Cleaner) kinavyoweza kufanya usafi kwa kufungwa kwenye treni  na  hivyo kusaidia  katika  kuzifanya njia za treni ( subways) kuwa katika    mazingira ya usafi  na hivyo kupunguza gharama za usafishaji.

Katika miaka sita tangu Rais Obama ambaye yeye binafsi amejipambanua kama mpenzi na shabiki mkubwa wa   sayansi na ubunifu, onyesho hilo limekuwa motisha na kivutio kikubwa kwa walimu, wanafunzi, wafadhili na  wataalamu waliobeba katika masuala ya  sayansi, teknolojia na   hesabu.
Kila mwaka  State dining room ya Ikulu hugeuzwa kuwa eneo la maeonyesho  ambapo  wanafunzi hujipanga na kuonesha vifaa walivyobuni au  kutoa maelezo ya kisayansi ya namna ya kutatua tatizo Fulani kwa kutumia teknolojia nafuu. 

Katika kutambua mchango wa Rais  Barack Obama katika kuwahamasisha wanafunzi  kupenda masomo ya  sayansi,   Ikulu  ya White House  imetangaza kwamba Kampuni ya Oracle inayojihusisha na  masuala ya teknolojia ya  Komputa katika miezi kumi na nane ijayo  itawekeza  dola za kimarekani 200 milioni kwaajili ya  masomo ya   sayansi ya computa   kwa wanafunzi wa kimarekani.

Katika maelezo yake kwa vyombo vya habari kabla na baada ya  kuhitikishwa kwa onyesho lake la mwisho, Rais Barack Obama amesema,  mara zote ambazo ameshiriki kujionea ubunifu wa vijana hao wadogo na wenye kiu na ari ya kuibua mambo mapya, amekuwa akijifunza kitu kipya na  mara zote amejiona  kama anayepungukiwa na kitu kutokana  kile anachojifunza kutoka  kwa wanafunzi hao.

“Nimeweza kujionea ubunifu  wa hali ya juu, kiu, na hamu ya    watoto na vijana wetu  wataalamu wa kesho wa taifa letu  la marekani.  Ipo siku huko mbeleni  nitajivunia pale ambapo miongoni mwa vijana wetu hawa watakapoweza kubuni tiba ya kansa. Nitaangalia  nyuma kwa fahari kubwa kwamba niliwawezesha vijana hawa kuibua vipaji vyao ”. Akasema Rais Obama kwa furaha   huku akiwashukuru wale wote ambao kwa miaka sita mfululizo wamewezesha kwa namna moja ama nyingine kufanyika  kwa onyesho  hilo.  

No comments:

Post a Comment