Monday, April 25, 2016

VIONGOZI WA UPINZANI NCHINI KENYA WAKABILIANA NA POLISI

Viongozi wa mrengo wa upinzani nchini Kenya (CORD) wamekabiliwa na maafisa wa usalama baada yao kuandamana hadi makao makuu ya Tume ya Uchaguzi (IEBC).
Maafisa wa usalama walianza kushika doria mapema asubuhi jumba la Anniversary Towers, lililo na afisi za IEBC.
Wabunge
Image captionWabunge wa CORD wamejiunga na viongozi wengine kuandamana
Viongozi wa Cord wakiongozwa na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga na waziri wa zamani wa mashauri ya kigeni Moses Wetangula walifika mwendo wa saa tano wakiandamana na mamia ya wafuasi lakini maafisa wa usalama wakawazuia kuingia katika afisi hizo.
Polisi
Image captionPolisi wametumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya
Mrengo huo unataka viongozi wa tume hiyo waondolewa.
Wanasema viongozi hayo hawawezi kutegemewa kuendesha uchaguzi mkuu huru na wa haki mwaka 2017.
Weta
Image captionBw Wetangula, aliye kiongozi wa chama cha Ford Kenya, ni mmoja wa viongozi walioshiriki
Viongozi wa CORD pia wamekuwa wakilalamikia kukataliwa kwa baadhi ya saini zilizowasilishwa na mrengo huo kuunga mkono ombi la kuandaliwa kwa kura ya maamuzi ya marekebisho ya katiba.
Mrengo
Image captionMrengo huo unasema hauna imani na IEBC
IEBC ilisema saini zilizokuwa halali hazikufika saini milioni moja zinazohitajika kikatiba ndipo ombi la marekebisho ya katiba kupitia kura ya maamuzi likubalike.

No comments:

Post a Comment