Wednesday, April 27, 2016

KIJIJI CHA NYEBURU CHAPATA MKOMBOZI WA MRADI WA UMEME WA VIJIJINIKIJIJI CHA NYEBURU CHAPATA MKOMBOZI WA MRADI WA UMEME WA VIJIJINI

Pic 17NA VICTOR MASANGU,
WAKAZI zaidi wa 100 katika kijiji cha Nyeburu Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani waliokuwa na tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme na kuishi katika giza kwa kipindi cha muda mrefu kwa sasa wamenufaika baada ya kuunganishiwa umeme kutokana na kukamilika kwa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu wa pili.

Baadhi ya wakazi hao ambao wamenufaika na mradi huo wakizungumza na na mwandishi wa habari hizi akiwemo Mguya Mvuti,Tina Emmanuel pamoja na Lamia Suka wamesema kwamba hapo awali walikuwa wanapata kero ya umeme na kusababisha kukwamisha shughui mbali mbali za kimaendeleo.
Aidha walisema kwamba kukamilika kwa mradi huo kutaweza kuleta chachu kubwa ya kimaendeleo katika kijiji hicho kwani mwanzoni wananchi hao walikuwa wanashindwa tutimiza malengo yao waliyojiwekea kutokana na kutokuwa na nishati hiyo ya umeme.
“Kwa kweli sisi kwa upande wetu kama wananchi wa kijiji hiki cha nyeburu hapo awali tulikuwa tunapata shida kubwa sasa nah ii yote ni kutokana tulikuwa tunaishi giza kipindi chote lakini kukamilika kwa maradi huu wa umeme vijijini hata kijiji chetu kitaweza kuapata maendeleo.

Kwa upande wake Meneja wa shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani Martin Madulu alisema kuwa kwa sasa wanatekeleza agizo lililotolewa na serikali kuhakikisha wanawafikia wateja wao wote hususan wale wa vijijini kwa lengo kuweza kuwaunganishia umeme kwa bei nafuu.
Aidha Madulu alisema kwamba kwa sasa watahakikisha wanafanya jitihaza za hali na mali katika kuwafikia wateja wao ili waweze kuwa na nishati ya umeme katika maeneo mbai mbali hususan kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya vijijini.
“Lengo letu kubwa kwa sasa tunatakeeza agizo lililotoewa na serikali na tumeshaanza katika maeneo ya Chalinze, Kisarawe na tutaendelea katika sehemu mbali mbali za Mkoa wetu wa Pwani na tunatarajia kufikia vijiji vipatavyo 109 vilivyopo katika Mkoa huu,”alisema Madulu.
Naye Mhandisi mkuu wa Miradi ya kupeleka umeme vijijini (REA) Mkoa wa Pwani Leo Mwakatobe amebainisha kuwa wanakumbana na changamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu yao hasa wakati wanapotaka kupitisha miundomibu katika makazi ya watu.
MRADI huo wa kusambaza umeme vijijini (REA) awamu ya pili katika Mkoa wa Pwani unatarajia kuvinufaisha vijiji vipatavyo 109,sawa na wateja 11000 ambapo utakamilika mwishoni mwa mwezi wa sita mwaka huu kwa gharama ya kiasi cha shilingi bilioni 30.

No comments:

Post a Comment