Monday, April 18, 2016

SINTOFAHAMU YAIBUKA MKATABA WA SOKO LA MACHINGA COMPLEX.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara  katika soko la machinga Complex  mara baada ya kutembelea na Kamati ya Ulinzi na Usalama  jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar eS Salaam, Paul Makonda (mwenye tinted kushoto)  akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wakitembelea soko la machinga Complex  jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar eS Salaam, Paul Makonda (mwenye suti mbele)  akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wakitembelea soko la machinga Complex  jijini Dar es Salaam.


SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema kuwa waliongia mkataba wa ujenzi wa soko la Machinga Complex unatatizo kutokana fedha nyingi kudaiwa  baada ujenzi sh.bilioni 36 huku ujenzi wa jengo hilo ni zaidi ya sh.bilioni 12.

Akizungumza  baada ya kutembelea jengo hilo Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, Makonda amesema kuwa kutokana hali hiyo anaunda kamati kuanzia kesho kuchambua mkataba huo kujua ni nani wamehusika na kwa nini waliingia au waliingia wakiwa wamekunywa pombe.

Amesema baada ya kuchambua wale waliohusika katika mazingira ya rushwa watachukuliwa hatua kutokana na kuiongezea mzigo serikali kwa masilahi yao.

Makonda amesema hata utaratibu wa ugawaji wa vizimba una matatizo kutokana baadhi ya watumishi wenye nafasi zao  kumiliki vizimba na kupangisha watu wafanyabiashara.

‘’Nitahakikisha mkataba wa machinga Complex una majibu ya kutosha juu ni nani waliohusika katika kubebesha mzigo serikali kwa wananchi wake’’ .amesema Makonda

Amesema katika mazingira hayo jengo hilo kwa fedha hiyo watu wafanyabiashara hawawezi kuilipa mpaka kuangaliwa uhalali wa mkataba wa ujenzi wa jengo hilo.

Aidha amesema kuwa wananchi wa Dar es Salaam lazima wachukie rushwa ili kuweza kupata huduma bora ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za rushwa na wanaotoa hata kama wanyonge hatua zitachukuliwa.

Amesema katika wafanyabiashara ndogo ndogo  wanaozungusha biashara zao katika mitaa waombe maeneo ya kufanyia kazi na kuweza serikali kupata kodi yake.

No comments:

Post a Comment