Showing posts with label Tanzania na Urusi. Show all posts
Showing posts with label Tanzania na Urusi. Show all posts

Thursday, April 28, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KWA RAIS VLADMIR PUTIN WA URUSI NA KUFUNGUA MKUTANO WA MAMBO YA FEDHA KWA WANAWAKE:

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia unga unaotokana na matunda ya mashelisheli pamoja na bidhaa mbalimbali za matumizi ya Nyumbani zinazofanywa na wajasiriamali wadogowadogo alipotembelea maonesho baada ya kufungua mkutano unaojadili kuhusu  mambo ya kifedha unaoangalia jinsi Mwanamke atakavyoweza kuingia kwenye mifumo yote ya kiuchumi hasa katika upatikanaji wa mikopo na mitaji kwa Mwanamke utakaorahisisha kufanya kazi zao kwa ufanisi. Mkutano huo umefunguliwa April 28,2016 katika Ukumbi wa BOT Dar es salaam.(Picha na OMR)