Wednesday, April 20, 2016

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAAFA.

C1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Maafa Zanzibar Ali Juma wakati alipofika katika Kambi ya Skuli ya Mwanakwerekwe C Wilaya Magharibi Unguja walipohifadhiwa   Wananchi  wa Shehia mbali mbali waliopatwa na maafa ya Mvua leo asubuhi.

C2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwaNd,Rahma Kassim Ali (katikati) Mkuu wa  Kambi ya Skuli ya Mwanakwerekwe C Wilaya Magharibi Unguja walipohifadhiwa   Wananchi  wa Shehia mbali mbali waliopatwa na maafa ya Mvua  wakati alipotembelea kambi hiyo leo asubuhi kuona hali halisi na huduma wanazopatiwa na Serikali.
C3Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Maafa Zanzibar Nd,Ali Juma Hamadi (kushoto)  wakati alipotembelea Kambi ya Skuli ya Mwanakwerekwe C Wilaya Magharibi Unguja walipohifadhiwa  Wananchi  wa Shehia mbali mbali waliopatwa na maafa ya Mvua  leo asubuhi kuona hali halisi na huduma wanazopatiwa na Serikali.
C6Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza familia za Wananchi  wa Shehia mbali mbali waliopatwa na maafa ya Mvua   katika Kambi ya Skuli ya Mwanakwerekwe C Wilaya Magharibi Unguja wakati alipofika kuwapa pole kutokana na maafa yaliyowapata leo asubuhi alipotembelea kambi hiyo.
C4Wananchi  wa Shehia mbali mbali waliopatwa na maafa ya Mvua   katika Kambi ya Skuli ya Mwanakwerekwe C Wilaya Magharibi Unguja wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akizungumza nao na kuwapa pole kutokana na maafa yaliyowapata wakati alipotembelea kambi hiyo leo asubuhi,
C5Watoto wa familia mbali mbali za Wananchi waliopatwa na maafa ya mvua wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza na Wazee wao wakati alipofika kuwapa pole kutokana na maafa yaliyowapata leo asubuhi alipotembelea kambi hiyo,
[Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment