Showing posts with label Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. Show all posts
Showing posts with label Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. Show all posts
Friday, April 29, 2016
Saturday, April 16, 2016
MPANGO WA KUHAKIKISHA KILA MWANANCHI ANATIBUWA KWA KUTUMIA BIMA YA AFYA KATIKA HOSPITALI MBALIMBALI KWA SHILINGI 40 KWA MWAKA:
Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, inayoongozwa na Chama cha Demkrasia na Maendeleo (Chadema), chini ya Ukawa imeanza kazi kwa staili ya aina yake baada ya kutangaza neema ya bima ya afya kwa wananchi wa Manispaa hiyo.
Imeahidi kuanzisha mpango maalum ambao kila mwananchi wa Manispaa hiyo atachangia Sh. 40,000 kwa mwaka ili aunganishwe na mpango wa matibabu wa bima ya afya ambao utawawezesha kupata matibabu ya bure katika hospitali mbalimbali.
Thursday, March 24, 2016
TUME YA UCHAGUZI YAKAMILISHA IDADI YA WABUNGE WA VITI MAALUMU WA TATU.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva akizungumza na waandishi wa habari na kutangaza Majina ya wabunge wa wa viti maalumu katika ukumbi wa tume ya uchaguzi jijini Dar es Salaam, kuhusiana na tume hiyo kukamilisha idadi ya wabunge watatu wa viti maalumu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wawili na wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema (Chadema) mmoja. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Givenes Aswile akiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa, Jaji Damiani Lubuva akitangaza majina ya wabunge wa viti maalumu watatu kuwa ni Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema). kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Emmanuel Kavishe.
Subscribe to:
Posts (Atom)



