Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Moovn Tanzania,Godwin Ndugulile akiangalia Aplikesheni ya Moovn Driver akiangalia simu mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Kulia ni Meneja wa kampuni hiyo,Ibrahim Ligonja na Kushoto niDereva ambaye wanajaribia simu yake kuangalizia Aplikesheni ya Moorn Driver, Masood Mohamed.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Moovn Tanzania,Godwin Ndugulile akionesha simu jijini Dar es Salaam jinsi Aplikesheni ya Moovn Driver inavyofanya kazi kati ya simu ya Dereva na Abiria. Kulia ni Meneja wa kampuni hiyo,Ibrahim Ligonja.
TANZANIA inatarajia kunufaika na teknolojia ya kisasa ya usafirishaji ya moovn Driver, kwa watu wanaohitaji kupiga simu ya mkononi kuhitaji usafiri.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo,Godwin Ndugulile amesema huduma hiyo itawasaidia madereva wa taksi, pikipiki na bajaji nchi kufanya biashara kwa wakati na kukuza kipato chao na nchi kwa kulipa kodi.
Amesema mtu atahitaji usafiri wa taxi au bodaboda, bajaji kwa nyakati tofauti ataweza kupata huduma hiyo kupitia teknolojia tuliyoibuni na kupelekwa popote katika hali ya usalama.
Ndugulile amesema kuwa dereva huyo kwa mfumo huo ataonekana kila sehemu atakapokwenda kupitia tekinolojia hii.
Amesema watumiaji satelaiti ambapo abiria atakapo kuwa akiiitumia kumtafuta dereva itamuonesha dereva aliyekuwa karibu yake na kuongeza kuwa endapo dereva huyo naye atakuwa akiitumia atapata taarifa kuwa katika eneo Fulani kuna abiria.
Alisema aplikesheni hiyo inapatikana bure kwa wateja wote ili kuweza kutoa huduma nafuu kwa vyombo vya usafirishaji mbalimbali kama taxi bodaboda, na bajaji.
Amesema madereva wataongeza kipato, watarahiaisha biashara, usalama dhidi ya mteja aliyempakia, mawasiliano, ripoti ya mapato na maripo ya kirahisi ya kulipwa kwa njia ya mtandao kupitia teknolojia hiyo.
Meneja wa kampuni hiyo,Ibrahim Ligonja, amesemaa kabla ya kuanza utaratibu huo waliishirikisha serikali na kuiingizia manufaa ya kupunguza uhalifu, uwezo wa kukusanya kodi sahihi ya mapato ya madereva na kuongeza kipato, kuhakikisha madereva wanafuata sheria na vibali na kurahisisha ajira.
No comments:
Post a Comment