Showing posts with label Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Show all posts
Showing posts with label Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Show all posts
Thursday, January 26, 2017
Thursday, December 15, 2016
Friday, November 11, 2016
MAKONDA AMWOMBA RAIS MAGUFULI KUTENGA ENEO LA KUZIKA VIONGOZI WA KITAIFA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemuomba Rais John Magufuli kutenga eneo katika makao makuu ya nchi yaliyopo mjini Dodoma, kwa ajili ya kuhifadhi miili ya viongozi waliotoa mchango wao katika kuliletea Taifa maeneleo .
Thursday, November 03, 2016
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ANATARAJIWA KUPANDA KIZIMBANI NOVEMBA 9 MWAKA HUU 2016
Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Novemba 9,2016 anatarajiwa kupanda kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujitetea dhidi ya kesi ya madai ya Sh 200
milioni iliyofunguliwa na waliokuwa makada wa CCM, Mgana Msindai na John
Guninita.
Siku
hiyo, Makonda anayetetewa na wakili wa kujitegemea, Seneni Mponda atatoa
ushahidi wa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Thursday, October 13, 2016
STEVE NYERERE STANDS UP COMEDY YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

Mchekeshaji Steve Nyerere akitoa burudani katika usiku wa Steve Nyerere Stand Up Comedy iliyofanyika Jumamosi Oktoba 8, 2016 ukumbi wa Little Theatre jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbali mbali waliweza kuhudhuria. Steve Nyerere amepanga kufanya onyesho la kuchekesha mara moja kwa kila mwezi ambapo mwezi ujao anatarajia kufanya onyesho hilo.
Friday, September 30, 2016
Tuesday, August 16, 2016
MAKONDA AYAOMBA MASHIRIKA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa wito kwa Taasisi na Mashirika mbalimbali jijini Dar es salaam kujitokeza kwa wingi kuunga mkono zoezi la uchangiaji wa hiari wa madawati kwa shule za msingi linaoendelea jijini humo ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia yatakayozalisha wanafunzi bora wa shule za msingi.
Saturday, June 25, 2016
MAGUFULI AWATAKA POLISI KUDHIBITI MAJAMBAZI NCHINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye uzinduzi wa kituo cha Mawasiliano cha Polisi Call Centre Biafra Kinondoni.
Thursday, June 16, 2016
Thursday, May 05, 2016
KUFIKIA MWAKA 2030 WAKAZI WA DAR WANATARAJIWA KUWA MILIONI 10:
MKOA wa Dar es Salaam unatarajiwa kuwa watu milioni 10 ifikapo 2030 hivyo kunahitaji uboreshaji wa jiji katika kuendana na idadi watu kuongezeka kwa kiwango kikubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda(Pichani) amesema kuwa kutokana kuwepo kwa ongezeko la watu kila mwaka Serikali ilibuni mradi wa uendelezaji wa jiji la Dar es Salaam kwa ufadhili wa Benki ya Dunia na serikali ya Tanzania.
Thursday, April 28, 2016
Saturday, April 16, 2016
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM NA KOREA KUSINI WAWEKA JIWE LA MSINGI LA HOSPITALI YA CHANIKA MANISPAA YA ILALA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) na Makamu wa Rais wa Shirika la Koica la nchini Korea Kusini, Taemyon Kwon, wakiweka tofali kwa pamoja kuashiria uweka wa jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika iliyopo Manispaa ya Ilala, inayojengwa kwa ufadhili wa nchi hiyo Dar es Salaam jana. Ujenzi huo hadi kukamilika utagharimu sh. bilioni 8.8 za kitanzania.
Hutuba na taarifa ya mradi huo zilisomwa.
Tuesday, April 12, 2016
Monday, March 28, 2016
YEYOTE ATAKAYE KIMBILIA KWENYE VYOMBO VYA DOLA KULISHITAKI KANISA ATAONA CHA MOTO:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema mkoa wake hauko salama kama watu wanavyodhani kwa sababu silaha nyingi zinamilikiwa kiholela na mafunzo ya matumizi ya silaha hizo hutolewa hata kwa watoto.
Makonda alisema hayo wakati wa ibada ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano na kuwataka wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kuhakiki silaha zao na kusalimisha zile zinazomilikiwa kinyume cha sheria.
Alisisitiza kwamba ifikapo Julai Mosi, operesheni maalumu ya kukamata silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria itaanza na yeye mwenyewe ndiye atakayeiongoza.
“Tumegundua kwamba kwenye bonde la mto unaotenganisha Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, kuna mafunzo yanatolewa kwa watoto. Wazazi wanadhani watoto wao wamekwenda shule kumbe wamechukuliwa huko.Hatuwezi kukubali hali hiyo iendelee."Alisema
Saturday, March 26, 2016
MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA AOMBEWA DUA NA MUFTI WA TANZANIA:
Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubery (wa pili kushoto), akimuombea dua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid na Msaidizi wa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Othman Mkambaku.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya kufanyika dua hiyo. Kushoto ni Mshauri Mkuu wa Mufti, Sheikh Abubakar Khalid.
Mufti Zubery, akifanya mazungumzo na Makonda.
Subscribe to:
Posts (Atom)





