Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akifafanua jambo wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) (hawapo pichani), kuhusu mkakati mpya wa Mamlaka hiyo wa kufanya kazi kwa ubunifu na uadilifu ili kuongeza mapato.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati alipozungumza nao kuhusu mkakati mpya wa Mamlaka hiyo wa kufanya kazi kwa ubunifu na uadilifu ili kuongeza mapato.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba, akitoa taarifa ya mafanikio ya Mamlaka hiyo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kulia waliokaa), akifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba, kuhusu matumizi ya mtambo wa kufuatilia miamala ya huduma za fedha inayofanyika kwa njia ya elektroniki kupitia simu za mkononi (TTMS).
Mtambo wa kufatilia miamala ya huduma za fedha inayofanyika kwa njia ya elektroniki kupitia simu za mkononi (TTMS).
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment