Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wadau waliopo chiniya wizara yake pamoja na watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Mara wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mkoa huo. Wengine pichani ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan(wa kwanza kulia),Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi.Anarose Nyamubi(wa tatu kulia) na Kaimu meya wa manispaa Bw.Wambura Kajala.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo amesema kuwa atahakikisha heshima ya tasnia ya habari inarudi baada ya kupitishwa kwa mswada wa sheria ya huduma za vyombo vya Habari.
Waziri Nape ameyasema hayo alipokuwa katika katika ziara mkoani Mara na Shinyanga na kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara hiyo na kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mikoa hiyo.
“Ule mswada utatoa tafsiri ya mwandishi wa habari,maana mwandishi wa habari lazma awe na sifa.Siku hizi anaweza kuwa mtu anauza ndizi alafu akajifunza kupiga picha akajiita na yeye mwandishi wa Habari.Ukifanya ivyo tasnia hii inakosa heshima,kwaiyo sheria ile itatafsiri nani mwandishi wa habari”Alisema Nape.
Aidha Waziri Nape alisema kuwa kwa kufanya hivi sheria hii itatibu tatizo la kulipwa vibaya na wamiliki wa vyombo vya habari maana mwandishi huyu atakuwa na elimu,maana kama hana elimu mmiliki ataajili mtu anaejua kusema wa kijuweni alafu ndo anamuajiri anakuwa mtangazaji wa radio yake kisa tu anajua kusema.
Pamoja na hayo waziri uyo mwenye dhamana ya wizara nyeti ya habari alisema kuwa sheria hiyo pia itazungumzia maslahi ya mwandishi wa habari,itawabana wamiliki na mswada huu ukipita utarudisha heshima ya tasnia hii ya habari katika nchi yetu.
Akizungumzia upande wa radio kujenga nchi waziri nape amewaasa waandishi wa habari na watangazaji wa radio kujenga amani ya nchi yetu kwa kuwaunganisha watanzania kupitia radio zao na si kuwatenganisha akitolea mfano wa yaliyotokea nchini Rwanda kwamba radio zilitumika kuhamasisha mauaji.
Mheshimiwa Nape pia amehaidi kuimarisha vitengo vya mawasiliano serikalini ikiwa ni pamoja na kuwapa maafisa hao vitendea kazi, pia ameliomba jeshi la polisi kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa na amehaidi kuzungumza na jeshi hilo ili waandishi hawa waweze kupata taarifa kirahisi.
Waziri uyo yupo katika ziara ya mikoa ya Kagera,Mara,Shinyanga,Tabora na Singida ikiwa na lengo kuu la kuileta Wizara ya habari,utamaduni,Sanaa na Michezo mikoani na wilayani karibu na wadau.
No comments:
Post a Comment