Sunday, April 17, 2016

MAMA WA MHARIRI MTENDAJI WA THE NEW HABARI ABSALOM KIBANDA AZIKWA RUNGWE MBEYA.


Familia ya wanahabari kutoka media mbalimbali pamoja na baadhi ya wahariri walioshiriki mazishi ya mama wa mhariri mtendaji wa The New Habari Absalom Norman Kibanda aliyesimama katikati mwenye miwani mara baada ya maziko yaliyofanyika Rungwe mission wilayani Rungwe mkoani Mbeya mchana.
Michuzi Media Group inakupa pole sana kwa msiba uliokupata mpiganaji Mwenzetu Absalom Kibanda,Tunaomba Mungu akupe uvumilivu wewe pamoja na ndugu wote katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu katika familia. Mungu alitoa na Mungu ametwaa jina la Bwana Lihimidiwe AMEN 

No comments:

Post a Comment