JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wapya
kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016 na kuwapangia vituo vyao vya kazi.
Makatibu Tawala
hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam na kisha
wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi
lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi.
Makatibu Tawala
walioapishwa ni;
1.
Arusha - Richard Kwitega
2.
Geita - Selestine Muhochi Gesimba
3.
Kagera - Armatus C. Msole
4.
Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour
5.
Pwani - Zuberi Mhina Samataba
6.
Shinyanga - Albert Gabriel Msovela
7.
Singida - Dr. Angelina Mageni Lutambi
8.
Simiyu - Jumanne Abdallah Sagini
9.
Tabora - Dkt. Thea Medard Ntara
10. Tanga
- Eng. Zena Said
Makatibu Tawala wengine
wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale waliohamishwa vituo vya kazi na wale
waliobaki katika vituo vya kazi walivyokuwep,o ambao tayari walishakula kiapo
cha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
27 Aprili,
2016
No comments:
Post a Comment