Tuesday, December 27, 2016

Polisi nchini Uganda wanasema takriban watu 30 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama katika ziwa Albert magharibi mwa taifa hilo. Abiria wengi walikuwa wanasoka na mashabiki wao waliokuwa wakielekea katika mechi ya kirafiki ya kuadhimisha siku ya Krismasi. Mafisa wa polisi wanasema chombo hicho kilikuwa kimejaa kupitia kiasi huku abiria wakiimba na kupiga tarumbeta. Boti hiyo inadaiwa kuzama katika maji yaliotulia . Ajali hutokea mara kwa mara katika ziwa Albert ,ambapo maboti hujaa kupitia kiasi licha ya kutofanyiwa ukarabati wowote.

ABODO AMSHAURI RAIS MAGUFULI AZIDI KUPUNGUZA BARAZA LA MAWAZIRI

 Mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo akizungumza nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki, ambapo alimtaka Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Rais John Magufuli azidi kupunguza Baraza la Mawaziri kufikia 15 na Kamati Kuu 15 pamoja na Halmashauri Kuu wajumbe 55.
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Jaffar Sabodo, amemshauri Rais John Magufuli kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri, akisema hali hiyo itamsaidia kuleta tija zaidi katika utendaji wake.

NAPE,MBOWE WAONGOZA KUUAGA MWILI WA MPOKI BUKUKU DAR

 Wanahabari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku baada ya kutolewa heshima za mwisho katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es Salaam, tayari kulisafirishwa kwenda kwao Msalato Dodoma kwa mazishi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

      

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU GHARAMA ZA MATIBABU YA DAWA YA SUMU YA NYOKA NCHINI

Kama tunavyofahamu, nchi yetu ina aina mbalimbali za nyoka ambao pindi wakimuuma mtu huleta madhara mbalimbali ya kiafya. Aidha tunafahamu kwamba tatizo hili lipo zaidi katika maeneo ya vijijini ambako uwezo wa wananchi kumudu gharama za matibabu ni mdogo.

Saturday, December 24, 2016

 Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Jaffar Sabodo akizungumza jijini Dar es Salaam, kuhusu wafanyabiashara wanaoficha fedha majumbani na kumshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
Sabodo akisisitiza jambo

Mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo (73), amemshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha ili kubana wafanyabiashara wakwepa kodi na kuficha fedha majumbani.

Aidha, amesema kutokana na utendaji wa Rais, haoni sababu za vyama vya upinzani kuendelea kumpinga, na badala yake waache siasa na waungane naye kujenga Tanzania mpya.

Kauli ya mfanyabiashara huyo iliungwa mkono na wachumi waliozungumza na gazeti hili kubainisha kuwa njia nzuri zaidi ni Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupunguza masharti kwa benki, hasa viwango vya riba, ili riba kwenye benki iwe kubwa jambo ambalo litafanya watu wakiweka fedha benki wapate faida.

Sabodo alitoa ushauri huo jana alipozungumza na JAMBO LEO katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Dar es Salaam, ambapo alisema licha ya hatua nzuri za Serikali ya Rais Magufuli kiuchumi na kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ubadhirifu na ufisadi, wapo walioficha mabilioni ya fedha nyumbani badala ya benki ili kukwepa kodi.

“Rais anafanya kazi nzuri, lakini ni wengi walioficha fedha nyumbani. Watanzania wanakufa njaa, wengine wameficha fedha. Hapo nashauri Rais abadilishe fedha hasa noti za Sh 5,000 na Sh 10,000. Hatua hiyo itasaidia kukabili ubadhirifu unaofanywa na watu wenye nia mbaya, lakini pia inaweza kuokoa uchumi na kufikia ndoto ya kuwa na Tanzania Mpya,” alisema Sabodo.

Aliongeza: “Kwa maoni yangu, hatua hiyo ya kubadilisha fedha ichukue kati ya mwezi mmoja na mmoja na nusu, watabainika wengi walioficha fedha nyumbani na hali ya uchumi itabadilika.”

Akifafanua, Sabodo ambaye ni mzaliwa wa Lindi, alisema India, Pakistan na Venezuela ziliwahi kukumbwa na hali kama iliyopo sasa nchini, lakini hatua ya kubadilisha noti ilizisaidia kuimarisha uchumi na bajeti zao.

“Watu wanaiba fedha nyingi, wanazificha chini ya magodoro, ili kumaliza hali hiyo ni muhimu noti zikabadilishwa hali itakayomlazimisha kila aliyeficha fedha kuzitoa, hapo wapo watakaokimbia nchi,” alisema Sabodo huku akitaja baadhi ya watakaokimbia hatua hiyo ikichukuliwa.

Sabodo alitoa kauli hiyo wakati Rais Magufuli ameshatoa kauli kuwataka walioficha fedha majumbani kuziacha ziingie kwenye mzunguko huku akionya wasipofanya hivyo anaweza kuamua kuzibadili ili wakose mahali pa kuzipeleka. 

Magufuli alitoa kauli hiyo Septemba kwenye mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi ambapo alisema watu hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa fedha zao benki na kuzificha kwa kuogopa kuwa atabaini kiasi walichonacho.

Wachumi
Akizungumzia suala hilo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (Sua), Profesa Damian Gabagambi alisema: “Kuendesha uchumi hakutakiwi nguvu sana. Uchumi unajengwa kwa imani, mtu yeyote anayeendesha uchumi anatakiwa kuijenga hiyo imani na ikuzwe.

“Chochote kinachofanyika na kuua imani kinavuruga uchumi, ukiona watu wanaficha fedha hilo si tatizo, ni kwamba kuna kitu ambacho ni tatizo, kuficha fedha ndio kujihami kwao.”

Alisema njia nzuri ya kufanya watu walioficha fedha kuzitoa, ni BoT kupunguza masharti inayowekea benki, hasa viwango vya riba, ili riba kwenye benki iwe kubwa, jambo ambalo litafawanya watu kutoficha fedha kwa maelezo kuwa wakipeleka fedha kwenye benki hizo, watapata faida.

Alisema riba inayotozwa kwenye benki inapangwa na BoT na kuitaka benki hiyo kufanya marekebisho ili kusaidia wanaoweka fedha kwenye benki kupata faida.

“Ila kama wana hakika fedha zimefichwa na wahusika hawawezi kuzitoa, njia pekee ni kutishia kuchapisha, ingawa hiyo ni njia ya haraka sana. Pamoja na hayo, muhimu ni kuhakikisha chanzo cha watu kuficha fedha kinajulikana,” alisema

Mhahidhi Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Haji Semboja alisema: “Katika uchumi ambao unakwenda vizuri na mamlaka zinazohusika na usimamizi wa fedha zinafanya kazi, suala hilo (kuficha fedha) haliwezi kujitokeza kwa maana mwenye fedha atajua jinsi ya kuziweka.

“Katika uchumi ambao watu wamekaa na kuhodhi fedha majumbani mwao ukitaka fedha hizo ziingie kwenye mzunguko basi unazibadilisha. Watu watazileta kwa nguvu maana hawatakuwa na ujanja. Ila kubadili fedha kuna sababu nyingi.”

Alisema sababu nyingine ni kutaka kubadili fedha ili kuwa na mwonekano mpya, pamoja na ubora wake ikiwa za awali zilikuwa zikichakaa mapema.

“Watu kukaa na fedha ndani ni kutoelewa mifumo ya kisasa ya kibiashara, watu wanaofanya hivyo ni wanaofanya shughuli ambazo haziko kwenye mfumo wa ulipaji kodi,” alisema.


Friday, December 23, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI MKUU MAJALIWA IKULU JIJINI DAR

Rais John Magufuli  akisalimiana na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKUU WA WILAYA YA UBUNGO ALAKIAPO LEO JIJINI DAR ES ESALAAM,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimwapicha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisari Matiku Makori kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni. Leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

RAIS MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NA PIA ATEUA MAJAJI

Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza uteuzi wa viongozi ya Tume ya Uchaguzi, Tume ya Maadili na Majaji wa Mahakama ya Rufaa Ikulu jijini Dar es salaam  Desemba 22, 2016.

Thursday, December 22, 2016

MACHINJIO YA KISASA YA SUNGURA KUJENGWA NCHINI.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Rabbit Republic ambaye ni mfugaji wa sungura kutoka Kenya, Moses Mutua (kulia) akielezea mipango yake ya kuzanzisha machinjio ya kisasa ya sungura hapa nchini, wakati wa hafla ya Kampuni ya Namaingo kugawa sungura kwa  vikundi 20 vya wajasiriamali, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Tuesday, December 20, 2016

SAA 144 ZA MAXENCE MELO NDANI YA MAHABUSU!

Maxence Melo akifikishwa mahakamani Ijumaa, Desemba 16, 2016. (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog).

Na Daniel Mbega
HATIMAYEasubuhi ya Jumatatu, Desemba 19, 2016 Maxence Melo ametoka kwa dhamana. Mungu ametenda.
Lakini ni baada ya Mkurugenzi huyo Mtendaji wa kampuni ya Jamii Media Limited inayomiliki mtandao maarufu wa JamiiForums, kusota mahabusu kwa takriban saa 144 – yaani saa 72 katika mahabusu ya polisi na saa 72 nyingine kwenye Gereza la Mahabusu la Keko.

SERIKALI YAIPONGEZA NAMAINGO KUGAWA MIRADI YA SUNGURA KWA WAJASIRIAMALI

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Bi Ubwa Ibrahim akihutubia wakati wa uzinduzi wa kugawa miradi ya sungura kwa wajasiriamali eneo la Majohe, Dar es Salaam.

Monday, December 19, 2016

MHE. DKT. POSSI AITAKA JAMII KUHESHIMU HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake katika shule ya Masasi yenye kuhudumia wenye ulemavu Mkoani Mtwara.

MAMA JANETH MAGUFULI AUNGANA NA WANAPAROKIA Wenzake kusali Ibada ya Jumapili Kanisa la Mt. Petro Dar es Salaam


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Friday, December 16, 2016

FAIDIKA YAZINDUA AINA MPYA YA MKOPO KUKUZA HUDUMA ZA KIBENKI NCHINI.






Afisa Mtendaji Mkuu wa Faidika, Mheshimiwa Mbuso Dlamini (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa chombo kipya cha mpango wa mkopo iitwayo 'Executive Loan' ambayo iliyoundwa kwa lengo la kurahisisha huduma za  kifedha na kulia ni Meneja Mauzo wa taasisi Nchini, Elisha Tengeni.



Afisa Mtendaji Mkuu wa Faidika, Mheshimiwa Mbuso Dlamini (kulia) akizindua mpango mpya wa mkopo iitwayo 'Executive Loan'

Thursday, December 15, 2016

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AKUTANA NA MACHINGA WA KARIAKOO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza nawafanyabiashara ndogo ndogo marufu kama Machinga mtaa wa Kongo na kusikiliza kero zao leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

MALARIA BADO NI GONJWA LINAOENDELA KUUA WATOTO WA CHINI YA MWAKA MMOJA KWA WINGI NCHINI.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam.

Monday, December 12, 2016

MZEE WA UPAKO: WOTE WALIONICHAFUA WATAKUFA MWAKANI......WASIPOKUFA NTAANZA KUUZA GONGO

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana amesema waandishi wote wa habari wanaoandika habari za kumchafua, watakufa kabla ya kufika Machi 2017.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa. 

VIDEO YA SHEREHE ZA MAULID ZILIVYOFANYIKA KITAIFA SINGIDA. MGENI RASMI ALIKUWA WAZIRI MKUU

Tazama  Hapa  Video  ya Sherehe  za  Maulid  Zilivyofanyika  Kitaifa  Singida. Mgeni   Rasmi  Alikuwa  Waziri Mkuu
 

Friday, December 09, 2016

Thursday, December 08, 2016

TAASISI YA AFRICAN RELIEF YAANZISHA KILIMO CHA UMWAKILIAJI CHUMBI, RUFIJI

Mkurugenzi wa Taasisi ya African Relief Organization, Samy  Mohammed Elazeb (kulia) akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.

Wednesday, December 07, 2016

WIZARA YA AFYA NCHINI YAPOKEA MSAADA WA AMBULANCE 10 TOKA SERIKALI YA QATAR

qatar
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto mapema leo imepokea jumla ya Magari 10 ya kubebea Wagonjwa (Ambulance) kutoka Serikali ya Qatar yaliyopokelewa na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Ummy Mwalimu Jijini Dar e Salaam 07 Desemba.2016.

MKUU WA NKOA WA DODOMA JORDAN RUGIMBA KONGAMANO LA WATU WENYE ULEMAVU

December  7 2016 mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana alikuwa ni mgeni rasmi katika kongamano la watu wenye ulemavu nchini ambapo katika hotuba yake aliwataka walemavu kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika mkoa ili kujikwamua kiuchumi huku akiahidi kuwasaidia mahitaji mbalimbali zikiwemo ofisi za kudumu.

Tuesday, December 06, 2016

BALOZI WA CUBA MHE. JORGE LUIS AMUAGA WAZIRI UMMY

6

Balozi wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Jorge Luis amuga Waziri wa Afya,maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na watoto Ummy mwalimu leo ofisini kwake,Balozi Luis amemaliza muda wake na hivyo kurejea nchini Cuba Waziri Ummy mwalimu amesema anaishukuru nchi ya Cuba kwa ushirikiano wao wa kuisaidia Tanzania kwenye sekta ya afya hususani kwenye mafunzo na kuleta madaktari kufanya kazi nchini Tanzania
(picha na Wizara ya Afya)

UHAKIKI WABAINI KAYA 55,692 HAZISTAHILI RUZUKU YA UMASIKINI

unnamed
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam kuhusu Kaya zilizoondolewa kwenye Mpango wa kunusuru Kaya Masikini (TASAF), Awamu ya Tatu kwa kukosa sifa. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ikulu, Bw. Peter Ilomo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, KATIBU MKUU PAMOJA NA NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

a1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakaribisha Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe  kabla ya kuanza kwa kikao chao cha pamoja na Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan.

WAZIRI MKUU AMALIZA MGOGORO WA SHAMBA LA MANYARA RANCH KWA KUKABIDHI HATI KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI,

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemaliza mgogoro wa ardhi  uliodumu kwa miaka 17 kati ya vijiji viwili vya Ortukai na Esilalei na Taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust (TLCT) baada ya kukabidhi hati ya  shamba la Manyara Ranch  kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Stephen Ulaya.
Hati hiyo imetolewa jana jioni (Jumapili, Desemba 4, 2016) na Waziri Mkuu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mto wa Mbu kwenye viwanja vya Barafu baada ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kwenda kwa wananchi wa vijiji  hivyo vilivyopo kwenye  Kata ya Elesilalei Wilayani Monduli Mkoani Arusha.

Monday, December 05, 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA ARUSHA, AANZA ZIARA YA MONDULI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwafariji wanawake waliolazwa kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakati alipotembelea wodi hiyo na kukuta wakiwa wamelala watatu kwenye kitanda kimoja.

SERIKALI YA AWAMU YA TANO INAONGOZWA KWA NGUVU ZA MUNGU

 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira pamoja na wachungaji, wakiinua mikono wakati wa ibada ya Kuliombea Taifa Kinziga, Salasala Jijini Dar es Salaam.

SEMENI LIKUNYWA POMBE GANI NA SEHEMU GANI

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake ameendelea kujibu madai hayo kwa mtindo wa ‘kudonoa donoa’ na jana aliwataka wanaodai kuwa alilewa siku hiyo wataje alikunywa pombe gani na katika baa gani. 

Wiki mbili zilizopita, taarifa kwenye vyombo vya habari zilisema kwamba Mchungaji Lusekelo alikwaruzana na majirani zake huku akidaiwa kuwa alikuwa amelewa jambo ambalo lilifanya achukuliwe na kuhojiwa na polisi. 

Saturday, December 03, 2016

CHUO CHA ARDHI CHATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI 104 WALIOFAULU

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Prof. Idrissa Mshoro (katikati kulia) akiteta jambo na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma), Prof. Gabriel Kassenga(katikati kushoto), pembeni kulia ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho (Mipango, Fedha na Utawala),Prof. Robert Kiunsi, pembeni kushoto ni Maafisa Waandamizi wa chuo hicho. Shughuli hizo zimefanyika  Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.

SEMINA YA LISHE NA AFYA YA JAMII IMEFANA BAADA YA WASHIRIKI KUPEWA SOMO JUU YA ULAJI UNAOFAA :


Kutoka kushoto ni mke wa askofu mkuu wa wapo mission international  Alhappynes Gamanywa na Elizabeth lyimo kutoka taasisi ya lishe na chakula.

PUMA YANG'ARISHA UTALII ZANZIBAR KWA MASHINDANO YA NDEGE KONGWE 22

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Rubani wa kike mdogo kuliko marubani wote wa ndege ya zamani, Sara Meehan (18), jinsi injini ya ndege hiyo kutoka Botswana inavyofanya kazi, wakati wa mapokezi  ya ndege hizo 'Vintage Air Rally' kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanznibar jana. Ndege hizo zilitengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930.

Friday, December 02, 2016

GODBLESS LEMA ANYIMWA DHAMANA KWA MARA NYINGINE TENA

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema. Mahakama hiyo imeeleza kuwa mawakili wamtuhumiwa huyo walipaswa kuonesha kusudio la kukata rufaa ndani ya siku10 kabla ya kukata rufaa.

WANAWAKE WAONGOZA KUWA NA VIRUSI VYA UKIMWI NCHINI

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Utafiti wa Viashiria vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na Maralia (THMIS) wa mwaka 2011/2012 kwa upande wa Tanzania Bara vinaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wameambukizwa ugonjwa huo kuliko wanaume.

DKT. MAGUFULI AMTEUA KAMISHNA WA MAGEREZA CP DKT. JUMA MALEWA KUWA KAMU MKUU WA JESHO LA MAGEREZA NCHINI TANZANIA








MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AENDESHA HARAMBEE YA SH.BILIONI 1 KUSAIDIA MFUKO WA UKIMWI NCHINI.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati akizundua Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Udhibiti Ukimwi (ATF)  Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA UMMA ARUSHA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na watumishi wa serikali na halmashauri wa mkoa wa Arusha kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha, Desemba 2, 2016.

Thursday, December 01, 2016

BALOZI WA KOREA KUSINI AENDESHA MHADHARA CHUO CHA BANDARI

Balozi wa Korea Kusini hapa nchini, Mhe. Song Geum-young (kushoto) akijadili jambo na Mkuu wa Chuo cha Bandari, Dk. Joseph Kakeneno wakati wa mhadhara wake na wanachuo cha Bandari hivi karibuni.

KAMISHNA WA TRA AHITIMISHA MAFUNZO YA ‘SCANNER’ MPYA BANDARINI

Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa mashine za ukaguzi wa mizigo ‘scanner’ kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na TRA. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Abdulrahman Mbamba pamoja na Wakufunzi kutoka Kampuni iliyofunga mashine hizo.