Mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo akizungumza nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, ambapo alimtaka Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais John Magufuli azidi kupunguza Baraza la Mawaziri kufikia 15 na Kamati Kuu 15 pamoja na Halmashauri Kuu wajumbe 55.
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Jaffar Sabodo, amemshauri Rais John Magufuli kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri, akisema hali hiyo itamsaidia kuleta tija zaidi katika utendaji wake.