Afisa Mtendaji Mkuu wa Faidika, Mheshimiwa Mbuso Dlamini (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa chombo kipya cha mpango wa mkopo iitwayo 'Executive Loan' ambayo iliyoundwa kwa lengo la kurahisisha huduma za kifedha na kulia ni Meneja Mauzo wa taasisi Nchini, Elisha Tengeni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Faidika, Mheshimiwa Mbuso Dlamini (kulia) akizindua
mpango mpya wa mkopo iitwayo 'Executive Loan'
Na Anasely Stanley,
Taasisi ya kibenki ya Faidika nchini,
imezindua aina mpya ya mkopo ijulikanayo kama ‘Executive Loan’, ikiwa na lengo
la kukuza utamaduni wa matumizi ya huduma za kibenki nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam jana, Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Bw. Mbuso Blamini,
alisema mkopo huo mpya unaendana na lengo chapa la taasisi la ‘kuboresha
Maisha’ ambao ni njia nyingine mpya kwa wateja ya uraisishaji wa shughuli zao
za kibenki.
“Leo ni siku kubwa katika historia ya
Faidika tukiwa tunazindua huduma mpya ya kifedha kutoka Faidika ambayo
inaendana na lengo chapa la taasisi yetu la “kuboresha maisha” ambayo ni
njia yetu mpya kwa wateja katika kuwaraisishia shughuli zao za kibenki kupitia
Executive Loan,” alisema Bw. Dlamini.
Bw. Dlamini alisema kuwa katika kipindi
cha miaka kumi ya Faidika, ikitoa huduma mbali mbali za kifedha kwa watu
wasiofikiwa zaidi na huduma hiyo katika imekuwa ndiyo chachu ya taasisi hiyo
kufikia lengo lake la kujenga taasisi iongozayo katika ushawishi wa kutumia
huduma za kibenki nchini.
“Tukizungumzia suala la ushawishi dhidi ya
matumizi ya huduma za kifedha, kama tunavyo hapa Faidika ‘Inclusive Finance’,
tunaelewa kuwa huduma za kifedha zinazidi kukua na ili kufikia lengo inatubidi
kuendelea kukidhi mahitaji yanazozidi kuongezeka kwa wateja wetu kwa kuwapatia
ya uraisishaji huduma kama hii ya Executive Loan ambayo imeundwa kipekee
kikidhi matakwa yao.
Tunajivunia kwa kupata nafasi
inayotustairi. Muhimu zaidi tumeweza kufanya hivyo tukiongozwa na misingi imara
ya utoaji wa huduma ya fedha rahisi, inayofaa na nafuu kwa zaidi ya watanzania
45,000 nchi nzima.
Executive Loan ni suluhisho la kiushindani
kwa soko la Tanzania, mkopo huo ukiwa hauna makusanyo ya ada au ada
zilizojificha,” alisema.
Mkopo huo umeandaliwa ili kuitikia matakwa
ya wateja kwa suluhisho ambalo limewalenga wateja ili kurahisisha shughuli zao
za kifedha.
“Tunaamini katika thamani itakayongeza,
ukiwa upatikanaji wake ni ndani ya masaa 48 na ulipaji wa mafungu ukiwa ni
zaidi ya miezi 72, mkopo wa juu zaidi ukiwa shilingi za kitanzania milioni 50;
ni mkopo wa aina ya kipekee Tanzania,” alibainisha.
Faidika ina wafanyakazi wa mauzo makini
ambao watawapatia wateja huduma kwa wakati wao na popote nchini, huku taasisi
hiyo ikiwa na idadi kubwa zaidi vituo vya mauzo nchini ikiwa na zaidi ya matawi
110.
Aidha, Faidika inatambua kuwa wateja wake
maalum hukosa muda, na hivyo benki imeweza kuwawekea watoa huduma maalum
watakao wapatia huduma hiyo kwa wakati wao na mahali popote nchini, na kukiwa
hakuna haja kwa mteja kutembelea ofisi za taasisi hiyo. “Hili linaendana na
lengo letu la kuwapatia wateja wetu huduma wakati wowote na mahali popote,”
alihitimisha.
No comments:
Post a Comment