Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na
Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay
Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam. wa kwanza kulia kwake ni Dada yake Ester Enock na anayefuata ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu Mama
Mary Majaliwa nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar
es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na baadhi ya waumini akiwemo muuza magazeti maarufu Bw. Bonge nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na baadhi ya waumini akiwemo muuza magazeti maarufu Bw. Bonge nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea komunyo kutoka kwa Padre Paul
Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es
Salaam.
Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli Jumapili ameungana na Wakristo wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu Petro iliyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki
kadhaa tangu alipougua na kulazwa hospitali.
Akiwa
mwenye afya njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa
Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wamesali ibada ya asubuhi katika
kanisa hilo na baadaye kusalimiana na waumini nje ya kanisa.
Baada
ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wameelezea
furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na
wamemuombea afya njema.
"Nimejisikia
furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya
njema na uso wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee
kumsimamia"
amesema Mama Mabula.
"Nimeshukuru
sana kumuona Mama yangu Mama Magufuli, Mwanajumuiya mwenzangu Kanisani, huku afya yake ikiwa imetengemaa zaidi, tunamshukuru sana
Mwenyezi Mungu na tunamuombea aendelee kumpigania afya yake izidi
kuwa imara"
amesema Thomas Simon.
"Kwa
kweli siku ya leo kwangu mimi ninafuraha sana kwa kumuona Mama akiwa
kanisani, na zaidi Mama wote wawili kwa sababu pia amekuja Mke wa
Mhe. Waziri Mkuu, kwa hiyo kwetu sisi ni furaha sana kama Parokia,
tunafurahi sana tunaposhirikiana na viongozi wetu"
ameongeza Epifania Ngonyani.
Mwezi
uliopita Mama Janeth Magufuli aliugua na kulazwa katika wodi ya
Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipata
matibabu kwa siku mbili na kisha kuruhusiwa.
No comments:
Post a Comment