WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 17 kati ya vijiji viwili vya Ortukai na Esilalei na Taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust (TLCT) baada ya kukabidhi hati ya shamba la Manyara Ranch kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Stephen Ulaya.
Hati hiyo imetolewa jana jioni (Jumapili, Desemba 4, 2016) na Waziri Mkuu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mto wa Mbu kwenye viwanja vya Barafu baada ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kwenda kwa wananchi wa vijiji hivyo vilivyopo kwenye Kata ya Elesilalei Wilayani Monduli Mkoani Arusha.
