Showing posts with label Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa. Show all posts
Showing posts with label Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa. Show all posts

Tuesday, December 20, 2016

SAA 144 ZA MAXENCE MELO NDANI YA MAHABUSU!

Maxence Melo akifikishwa mahakamani Ijumaa, Desemba 16, 2016. (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog).

Na Daniel Mbega
HATIMAYEasubuhi ya Jumatatu, Desemba 19, 2016 Maxence Melo ametoka kwa dhamana. Mungu ametenda.
Lakini ni baada ya Mkurugenzi huyo Mtendaji wa kampuni ya Jamii Media Limited inayomiliki mtandao maarufu wa JamiiForums, kusota mahabusu kwa takriban saa 144 – yaani saa 72 katika mahabusu ya polisi na saa 72 nyingine kwenye Gereza la Mahabusu la Keko.