Kutoka kushoto ni mke wa askofu mkuu wa wapo mission international Alhappynes Gamanywa na Elizabeth lyimo kutoka taasisi ya lishe na chakula.
Washiriki wa semina wakifuatilia semina kwa makini.
Mwalimu Elizabeth Lyimo Akifundisha katika semina.
Magonjwa
yasioambukizwa yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana katika jamii kutokana na
ulaji wa vyakula usiofaa
Kauli hiyo
imetolewa na elizabeth lyimo kutoka taasisi ya lishe na chakula jijini dare s
wakati akifundusha katika semina chakula na lishe iliyoandaliwa na taasisi hiyo wakishirikiana na wapo misssion
international jijini dares salaam
Ambapo
alisema kuwa ni vyema jamii kupewa elimu ya kutosha juu ya chakula maana
watanzanaia wengi wanapenda kufuata taratibu ila shida ni elimu
Aidha
amesema kuwa kwasasa ni mtindo bora wa maisha ambapo kuna mitindo mingi kama
vile kuvuta sigara kunywa pombe kula chumvi kwa wingi matumizi ya tumbaku
,ulaji usio faa na teknolojia uambayo imeongezeka.
Aliongeza
kuwa kama serikali inajitahidi kutoa elimu kwa jamii na kuwasihi jamii kufanya
juhudi ya kutafuta elimu juu ya lishe inayofaa na kufuata maelekezo kutoka kwa
wataalamu na kufanyia kazi yale ambayo wamejifunza.
kwa upande
wake mwandaaji wa semina hiyo ya chakula na lishe Ndugu Respicius Mweisiga amewasihi jamii kubadilisha mfumo wa ulaji
ambapo alisema kuwa ni vyema jamii ibadilike na kuanza kula na kutumia vyakula
vya asili.
Hata hivyo
Bwana Mweisiga alisema kuwa kutokana na matatizo ya ulaji sasa ni wakati wa
jamii kujifunza na kutumia vyakula vya asili
Katika
semina hiyo waliohudhuria wamejifunza mtindo wa maisha na ulaji
unaofaa,Piramidi ya chakula,madhara yatokanayo na ulaji usiofaa magonjwa kama
vile kisukari,moyo,shinikizo la damu,saratani nk,umuhimu wa mazoezi na kuzuia
utapiamlo.
No comments:
Post a Comment