Wednesday, December 07, 2016

WIZARA YA AFYA NCHINI YAPOKEA MSAADA WA AMBULANCE 10 TOKA SERIKALI YA QATAR

qatar
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto mapema leo imepokea jumla ya Magari 10 ya kubebea Wagonjwa (Ambulance) kutoka Serikali ya Qatar yaliyopokelewa na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Ummy Mwalimu Jijini Dar e Salaam 07 Desemba.2016.

Awali kabla ya kupokea magari hayo ya kubebea wagonjwa, yaliyokabidhiwa na Mwakilishi wa Serikali ya Qatar hapa nchii, Balozi wa Qatar, Mh. Abdulla Al Suwaid,  Waziri Ummy Mwalimu alimwakikishia Balozi huyo kuwa Wizara yake itayatunza magari hayo na yatafanya kazi iliyokusudiwa huku kipaumbele yakipelekwa katika maeneo yenye uhitaji wa haraka.
“Tunashukuru Serikali ya Qatar kwa kuendelea kushirikiana nasi katika hili. Tunawahakikishia magari haya tutayatunza na yataenda kwenye maeneo yote kusudiwa na kipaumbele zaidi ni pamoja  kwenda kusaidia Wanawake Wajawazito.
Pia mbali na Wanawake Wajawazito na Watoto magari haya yataenda katika maeneo yenye uangalizi maalum ikiwemo yale yenye kutokea ajali za mara kwa mara.” Alieleza Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha, Magari  hayo yanatrajiwa kwenda katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Morogoro, Tanga, Tabora, Kagera pamoja na maeneo ya mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo wameona kuna umuhimu zaidi. Pia kwa Dar es Salaam magari hayo mengine yatapelekwa Wilaya ya Kigamboni na lingine katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo yatasaidia kusafirisha wagonjwa kutoka Hospitalini hapo kwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya safari za matibabu.
Kwa upande wake Balozi wa Qatar amebainisha kuwa, Serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana a Tanzania katika kuimalisha mambo mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya.

Qatar
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akielezea jambo mbele ya waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa tukio hilo. kushoto kwake ni Balozi wa Qatar nchini Mh. Abdulla Al Suwaid
dsc_0819
Balozi wa Qatar nchini Mh. Abdulla Al Suwaid akisoma taarifa fupi wakati wa kukabidhi magari hayo kwa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto  iliyowakilishwa na  Mh. Ummy Mwalimu.
dsc_0833
dsc_0835
Balozi wa Qatar nchini Mh. Abdulla Al Suwaid akimkabidhi moja ya funguo ya gari la wagonjwa (Ambulance) Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu
qatar
ummy mwalimu
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akimkabidhi funguo mmoja wa wawakilishi ambapo magari hayo yatapelekwa
dsc_0850
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akifunguliwa mlango wa moja ya Ambulance zilizokabidhiwa kutoka Serikali ya Qatar
dsc_0849
Baadhi ya wawakilishi ambapo magari hayo yatapelekwa wakiwa na wakionyesha juu funguo za Ambulance  baada ya kukabidhiwa na Waziri ummy Mwalimu.
dsc_0846
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akikabidhi funguo hizo
dsc_0843
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akikabidhi funguo hizo
dsc_0839
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akipokea funguo 10  za Ambulance baada ya kukabidhiwa kutoka kwa Balozi wa Qatar
dsc_0861
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akikagua maeneo ya ndani ya Ambulance hiyo mara baada ya kukabidhiwa.
dsc_0874
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akiwa ndani ya upande wa dereva baada ya kukabidhiwa. 
dsc_0877
Moja ya Ambulance zilizokabidhiwa na Serikali ya Qatar
dsc_0883
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akikabidhi funguo kwa moja ya wawakilishi wa mikoa ambao gari hizo zitakazo kabidhiwa.
dsc_0892
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii  Jinsia Wazee na Watoto. Mh. Ummy Mwalimu akiwa na Balozi wa Qatar nchini Mh. Abdulla Al Suwaid mara baada ya kukabidhiwa magari hayo.

No comments:

Post a Comment