Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Rubani wa kike mdogo kuliko marubani wote wa ndege ya zamani, Sara Meehan (18), jinsi injini ya ndege hiyo kutoka Botswana inavyofanya kazi, wakati wa mapokezi ya ndege hizo 'Vintage Air Rally' kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanznibar jana. Ndege hizo zilitengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930.