Showing posts with label Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC). Show all posts
Showing posts with label Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC). Show all posts

Monday, December 12, 2016

MZEE WA UPAKO: WOTE WALIONICHAFUA WATAKUFA MWAKANI......WASIPOKUFA NTAANZA KUUZA GONGO

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana amesema waandishi wote wa habari wanaoandika habari za kumchafua, watakufa kabla ya kufika Machi 2017.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa. 

Monday, December 05, 2016

SEMENI LIKUNYWA POMBE GANI NA SEHEMU GANI

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake ameendelea kujibu madai hayo kwa mtindo wa ‘kudonoa donoa’ na jana aliwataka wanaodai kuwa alilewa siku hiyo wataje alikunywa pombe gani na katika baa gani. 

Wiki mbili zilizopita, taarifa kwenye vyombo vya habari zilisema kwamba Mchungaji Lusekelo alikwaruzana na majirani zake huku akidaiwa kuwa alikuwa amelewa jambo ambalo lilifanya achukuliwe na kuhojiwa na polisi.