Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
(katikati) akisalimia wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya
Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wao wa mwaka Uliofanyika
Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma tarehe 19 Januari, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akizungumza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa Chama
cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu Januari 19,2017 katika Ukumbi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
Baadhi ya wajumbe Chama cha Akiba
na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa kwanza wa mwaka
Januari 19, 2017 Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya Utawala na
Usimamizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchasi
akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wanachama wa Akiba na
Mikopo wa Ofisi hiyo Mkoani Dodoma Januari 19, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
akikabidhi ada ya uanachama na hisa zake kwa Katibu wa chama Bi.
Algensia Ngalapa mara baada ya kuamua kujiunga rasmi na Chama cha Akiba
na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Mkutana wao Januari 19, 2017
Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Akiba na
Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Joseph Muhamba akitoa neno la shukrani
kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu
wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Mkutano wa chama hicho
mkoani Dodoma tarehe 19 Januari, 2017.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
(watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza wakati wa
mkutano wa Wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Ofisi ya Waziri
Mkuu kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano hiyo Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (wa
pili kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama
wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Ofisi ya Waziri Mkuu, Kulia kwake ni
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri (watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah
Possi na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Joseph Muhamba.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
…………………………………………………………..
Na mwandishi wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
ameshauri uongozi wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Ofisi ya Waziri Mkuu
(Makamu Saccos) kuwa na ubunifu katika utendaji ili kuleta manufaa zaidi
kwa wanachama wake.
Mhe. Mhagama ameyasema hayo
wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanachama wa Chama hicho
uliofanyika Januari 19, 2017 mkoani Dodoma.
Katika Mkutano huo Mhe. Waziri
alisisitiza kuwepo na mikakati madhubuti ya kubuni miradi itakayowezesha
chama kuwa na vyanzo vyake vya mapato na kuwa na mikakati ya kuongeza
wanachama wapya kwa kuzingatia umuhimu wa chama hicho.
“Ni muhimu kuwa na mikakati
madhubuti ya kubuni miradi, kuongeza wanachama pamoja na kuwa na vitu
vya kiupekee na vya kiufanisi vitakavyokisaidia chama kuwa imara katika
utendaji wake”, alisema Waziri Mhagama.
Aliongeza kuwa chama hicho
kimekuwa msaada mkubwa kwa wanachama wake amabapo wengi wao wamekuwa na
maendeleo mbalimbali kutokana na uwepo wa fursa za mikopo isiyokuwa na
masharti magumu.
“Chama kimekuwa mkombozi mkubwa
kwa wanachama wake kwani wamekuwa wakikopa na kusaidia katika shughuli
za kimaendele, ikumbukwe kuwa asilimia kubwa ya wafanyakazi wana
maendeleo kwakuwa wanachukua mikopo mbalimbali inayowasaidia kuwepo na
maendeleo ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja”, alisisitiza Mhe.Mhagama.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Chama hicho Bw. Joseph Muhamba aliahidi kuyachukua mapendekezo yote
yaliyotolewa na Mhe.Waziri na kuyaweka katika vitendo ili kuhakikisha
chama kinaongeza mbinu za ubunifu ikiwemo eneo la kuongeza wanachama
wapya na kuweka mazingira mazuri zaidi kwa wanachama waliopo.
Mhe. Mhagama aliahidi kutoa
ushirikiano wake kwa Chama hicho na kueleza kuwa chama kiitumie fursa ya
Serikali kuhamia Dodoma kama chachu ya kuongeza wanachama wapya.
“Ninawaahidi kuwapa ushirikiano
wa hali na mali na kuamini kuwa chama hiki ni msaada mkubwa kwa
wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwani kipo kisheria kabisa na zipo
kanuni zinazoelekeza juu ya uwepo wa chama na kwa kuonesha mfano mimi na
Naibu Waziri Mhe. Dkt. Possi tunajiunga rasmi hii leo ili kuwa mstari
wa mbele kukisaidia chama hiki”. Alisema Mhe. Mhagama.