Jeshi la polisi mkoa wa Arusha, linawashikilia Askari wanne wa SUMA JKT kwa tuhuma za kuhusika kuwaua wafugaji wanne kwa kuwapiga risasi na kuwajeruhi wengine watano kwenye vurugu zilizotokea eneo la Oldobnyo Sambu wilayani Arumeru.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema chanzo cha mauaji hayo ni wafugaji wa kimaasai kuwavamia askari hao ambao walikuwa wamekamata ng’ombe ambao waliingizwa ndani ya msitu wa hifadhi ambao ni wa serikali, kwa ajili ya malisho, kutokana na ukosefu wa malisho.

