Showing posts with label Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Show all posts
Showing posts with label Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Show all posts

Sunday, January 22, 2017

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA GEREZA LA RUANDA JIJINI MBEYA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiongozana na Mkuu wa Jeshi la Magereza jijini Mbeya Kamishna Msaidizi Paul Kajida (kulia) wakati alipowasili kukagua shughuli za uzalishaji thamani za ndani na sabuni katika gereza la Ruanda .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.

Friday, October 07, 2016

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA CZECH ATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni(kulia), akimsikiliza Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek wakati wa mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia njia za mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu.Mazungumzo yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam. 

Thursday, June 23, 2016

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI AZUNGUMZIA MATUKIO YA KIHALIFU YALIYOTOKEA MKOA WA KUSINI PEMBA


Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba, mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba na kuahidi kuyashughulikia. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omary Makame.

Tuesday, March 15, 2016

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI MHANDISI MASAUNI AMPOKEA WAZIRI MKUU NA KUTEMBELEA KAMBI YA MWISA:

1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa alipotembelea Kambi ya Utenganisho ya Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera, kambi hiyo inahifadhi wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi kwa sababu za kiusalama.

2
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa(kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya wakimbizi,iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke. Waziri Mkuu alitembelea Kambi ya Utenganisho ya Mwisa,iliyoko wilayani Misenyi,mkoani Kagera, kambi hiyo inahifadhi wakimbizi waliotengwa kutoka katika makambi ya wakimbizi kutoka nchini Burundi kwa sababu za kiusalama.