Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe Angellah Kairuki(kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya
kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza kwa makini
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt.Henry Mambo wakati
alipokuwa akiwaelezea maadeleo ya ukarabati wa majengo ya chuo hicho
tawi la Magogonijijini Dar es Slaam, kamati ya bunge ilifanya ziara ya
kikazi katika chuo hicho.
Kaimu
Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt.Henry Mambo,
akisisitiza jambo mbelea ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kamati
hiyo , Jasson Rweikiza,anayefuata ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki na
kwa kwanza kulia ni Suzan Mlawi, Naibu Katimu Mkuu wa Wizara hiyo ya
Ofisi ya Rais.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe Angellah Kairuki (kulia) akifafanua jambo kwa wajumbe wakamati ya
kudumu yabunge ya Utawala na Serikaliza Mitaa wakati walipofanya ziara
ya kikazi katika makao makuu ya chuo hicho,Mtaa wa
Bibi Titi, jijini Dar es Salaam, jana .Katikati ni Mwenyekiti wa kamati
hiyo , Jasson Rweikiza na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishiwa Umma
Dkt.Henry Mambo.
Meneja
Uhusiano wa Kampuni ya Ino Communications Barnabas Lugwisha,
akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki wakati wa ziara hiyo jana
Chuo cha Utumishi wa Umma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe Angellah Kairuki amesema kwamba serikali kupitia Chuo Cha Utumishi
wa Umma Tanzania (TPSC) itaendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Umma
ili waendane na kasi ya mabadiliko, changamoto na mahitaji ya sasa
katika utumishi wa Umma.
Akiwasilisha
taarifa ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania mbele ya Kamati ya Kudumu
ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa Makao Makuu ya TPSC Mtaa wa
Bibi Titi Jijini Dar es Salaam , Waziri Kairuki alisema kuwa mafunzo
hayo ni muhimu sana kwa watumishi hao.
Aliongeza kuwa pia serikali inakamilisha mchakato wa mandalizi ya mafunzo ya lazima kwa watumishi wa umma nchini.Katika
kuongeza ufanisi na tija wa chuo hicho, chuo kimejenga, kuhuisha na
kusimika mifumo mbalimbali ya kusimamia utekelezaji wa majukumu.
“Baadhi
ya mifumo hiyo ni mpango mkakati mwa mwaka 2016-2021,utekelezaji
kikamilifu kwa mkataba wa huduma kwa mteja na kuanzishwa kwa dawati la
malalamiko na kamati za uadilifu.Waziri
alisema majukumu mengine ni kuendelea kusimika mifumo ya Tehema,
miundombinu ya mtandao (LASN) , Mtandao wa serikali (Govnet) , mfumo wa
simu za serikali (Voip) na mfumo wa barua pepe za Serikali (GSM).
Waziri
Kairuki aliiambia kamati hiyo kuwa katika kuendeleza weledi wa
watumishi wa Umma katika utunzaji wa kumbukumbu na Uhazili, Chuo
kinatarajia kuanzisha shahada ya kwanza katika maeneo hayo mawili.“Rasimu
ya Mitaala hiyo, imeshaandaliwa na kuwasilishwa baraza la Ithibati na
Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa ajili ya uhakiki na kuidhinishwa.”
Alisema
pia kuwa TPSC hutoa ushauri wa kitaalam kwa Wizara, Idara, Wakala za
Serikali , Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta binafsi.Baadhi
ya shauri hizo za kitaalam ni katika maeneo ya miundo na mifumo ya
utumishi , mpango mkakati ,Mkataba wa huduma kwa mteja , tathmini na
uchambuzi kazi , tathmini ya utoaji huduma katika utumishi wa umma na
usimamizi wa mchakato wa ajira.
Waziri
aliyataja baadhi ya majukumu ya Chuo kuwa ni kutoa mafunzo ya muda
mfupi kwa watumishi wa wa umma ili kuwajengea uwezo katika kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi. Mafunzo hayo ni katika Nyanja mbalimbali
zikiwemo menejimenti ya usimamizi na rasilimali watu, menejimenti,
uongozi na utawala, utunzaji wa kumbukumbu na usimamizi wa fedha .
Pia
kinatoa mafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya cheti na stashahada
katika maeneo ya menejimenti na utawala, utunzaji wa kumbukumbu na
uendeshaji wa ofisi, mafunzo ya uhazili,usimamizi wa fedha za umma ,
ununuzi na ugavi,huduma za maktaba utawala wa serikali za mitaa, sheria
na teknolojia ya habari na mawasiliano.
Chuo kina matawi sita mbayo ni Dar es Salaam, Mtwara, Tabora, Singida Tanga na Mbeya.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali
za Mitaa, Jasson Rweikiza (MB-Bukuba Vijijini) alikipongeza chuo hicho
kwa jitihadaza zake za kuwaendeleza watumishi wa Umma na kutoa ushauri
kwa Serikali ifungue tawi la chuo hicho Jijini Mwanza, ili kuwahudumia
wakazi wa kanda ya Ziwa.
No comments:
Post a Comment