Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe.
Semistocles Kaijage (wa tatu kutoka kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa
Tume Jaji Mst. Zanzibar, Hamid M. Hamid (wa tatu kutoka kulia) wakiwa
katika picha ya pamoja na watendaji wa NEC walipotembelea vituo vya
kupigia kura katika Jimbo la Dimani kuangalia maandalizi ya Uchaguzi
mdogo wa Ubunge utakaofanyika Jumapili, Januari 22, 2017.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe.
Semistocles Kaijage (kushoto) akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Huduma
za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe akiwasili katika kituo cha
kupigia kura cha Skuli ya Maandalizi na Msingi Dimani, Zanzibar kukagua
kukamilika maandalizi ya Uchaguzi wa Ubunge katika jimbo hilo leo. Kulia
ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani bi. Idaya Seleman
Hamza.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe.
Semistocles Kaijage (kulia) akiangalia Orodha ya majina ya wapiga kura
603 iliyobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi
ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani Zanzibar leo. Wengine ni Mkurugenzi
wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (katikati) na Msimamizi
Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
Mkurugenzi
wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (katikati) akimweleza
jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe.
Semistocles Kaijage (kushoto) alipotembelea kituo cha kupigia kura cha
Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani leo. Kulia
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman
Hamza.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe.
Semistocles Kaijage (kulia) akiangalia Orodha ya majina ya wapiga kura
603 iliyobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi
ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani Zanzibar leo. Kulia ni Msimamizi
Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mst. Zanzibar, Mhe.
Hamid M. Hamid (katikati) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) na
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe mara baada
ya kutembelea kituo cha kupigia kura cha Dimani leo visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe.
Semistocles Kaijage akizungumza na Watendaji wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi leo mara baada ya kutembelea vituo vya kupigia kura katika
jimbo la Dimani. Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu
wa Zanzibar, Hamid M.Hamid (wa pili ), Msimamizi Msaidizi wa jimbo la
Dimani Bi. Idaya Selemani Hamza (katikati), Mkurugenzi wa huduma za
kisheria, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia).
Orodha ya
Majina ya Wapiga kura iliyobandikwa Siku nane kabla ya Uchaguzi mdogo
wa Ubunge katika kituo cha kupigia kura cha Nyamanzi chenye wapiga Kura
603 katika jimbo la Dimani leo.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe.
Semistocles Kaijage (Kulia) akimweleza jambo Mkurugenzi wa Huduma za
Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emanuel Kawishe (kushoto) mara
baada ya kukagua mabango ya Matangazo ya Tume kuhusu upigaji wa kura,
Orodha ya Majina ya Wapiga kura na wagombea katika kituo cha kupigia
kura cha Skuli ya Maandalizi Kisakasaka, Dimani Zanzibar leo.
Moja ya
Tangazo la Elimu ya Mpiga Kura linaloonyesha utaratibu wa kufuata wakati
wa kupiga Kura lililobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha
Kisakasaka katika jimbo la Dimani.
No comments:
Post a Comment