Showing posts with label Waziri wa Fedha na Mipango. Show all posts
Showing posts with label Waziri wa Fedha na Mipango. Show all posts

Tuesday, January 31, 2017

SERIKALI YAELEZA UTEKELEZAJI WA MASUALA MBALIMBALI BUNGENI

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwasilisha kauli ya Serikali kuhusu Mwenendo wa Hali ya Uchumi wa Taifa, Bungeni Mjini Dodoma.

Friday, June 10, 2016

SERIKALI YAPATA GAWIO LA SH. BILIONI 23 KUTOKA KAMPUNI ZA PUMA ENERGY, TIPER (T) NA NMB BANK PLC

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Mpango (Mb), akipokea hundi kifani yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.5 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Puma Energy Dkt. Ben Mosha, wakati wa Hafla fupi ya serikali kukabidhiwa Hundi za Mfano zenye thamani ya shilingi Bilioni 23 kutoka kwa Kampuni za Puma Energy, Tiper (T) na NBC Bank PLC, ambazo imewekeza hisa zake, katika ukumbi wa Hazina (Treasury Squire) Mjini Dodoma

Monday, May 02, 2016

SERIKALI KUTUMIA SHILINGI BILIONI 59.5 KUWEZESHA VIJIJI NCHI NZIMA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dokta Philip Mpango, amesema kuwa serikali imepanga kutumia shilingi 59.5bn kwaajili ya kuviwezesha vijiji nchi nzima katika kipindi cha mwaka fedha 2016/2017

Dokta Mpango, aliwaambia wabunge mjini Dodoma, leo tarehe 30, Machi, 2016, kwamba fedha hizo ni kwajili ya kukiwezesha kila kijiji shilingi 50m kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali.

Sunday, April 24, 2016

SERIKALI YAWAKALIA KOONI WATUMISHI WAZEMBE NA WABADHILIFU:


Serikali imesema kuanzia sasa mtumishi wa umma atakayeshindwa kusimamia rasilimali za umma, achague moja kati ya mawili, kuacha kazi au atumbuliwe.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango wakati alipozindua kitabu cha mwongozo wa usimamizi wa rasilimali za umma unaolenga kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa na kusimamiwa vizuri kwa maslahi ya Taifa.