Waziri
wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
katikati akikata utepe kuashiria kuzindua mradi wa Mkunga Okoa Maisha ,
wa kwanza kushoto ni Balozi wa Canada Bi. Susan Steffan na wakawnza
kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wakunga nchini Dkt. Sebalda Leshabari.
Waziri
wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiongea na wadau wa Baraza la Baraza la Wakunga hawapo pichani wakati
wa kuzindua mradi wa Mkunga Okoa Maisha kwa kushirikiana na watu wa
Canada.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
ametoa agizo kwa viongozi wote nchini kuacha mara moja kuwakamata
wauguzi, wakunga na kuwaweka ndani na badala yake wanapaswa kufuata
taratibu zilizopo.
Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa
mradi wa Mkunga Okoa Maisha Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema wakunga wanalo baraza ambako
ndilo suluhishi la matatizo yao.
"Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa
pale ambapo muuguzi au mkunga anapokosea zipo taratibu za kufuata na
siyo kumweka ndani kwani kuna Baraza la Wakunga ambalo lina Mamlaka ya
kisheria za kuchukua kwa mkunga yoyote ambaye amekwenda kinyume.
"Tunao
Wakunga na wauguzi ambao wanafanya kazi zaidi ya masaa, tumeona
kilichotokea Sikonge, kiongozi anakuja juu kwanini mtoto amepewa dawa ya
Quinn," alisema Ummy.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Wakunga nchini Dkt. Sebalda
Leshabari amesema kuwa mradi huo unalenga kupunguza vifo katika Mikoa
ya Shinyanga na Simiyu hivyo wauguzi na wakunga ni vema wakashirikiana
na Baraza hilo ili kufanikisha malengo yao.
No comments:
Post a Comment