Thursday, January 26, 2017

MAKONDA AKUTANA NA MADEREVA TAX

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza  na Umoja wa Madereva Tax na kusikiliza kero zao, jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wamiliki wa Tax Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Ashiru akifafanua jambo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZTO) ACP Awadhi Haji akitoa elimu kwa madereva wa Madereva Tax leo jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul  Makonda amekutana  na Umoja wa Madereva Tax Wilaya ya Ilala ilikusikiliza  kero zao zinazowakabili katika kazi yao.

Makonda ameyasema hayo leo alipokutana na madereva hao, amesema kunahitaji madereva wa tax kuwa mfumo bora wa kusaidia jiji la Dar es Salaam kuwa na huduma bora ya usafiri wa tax na wenye usalama

Amesema ni vyema kukawepo kifaa maalum kitakachoonesha umbali wa mteja anapokwenda ili alipe kulingana na umbali huo na ajue bei hiyo kuliko kukadiriana, pia amesema katika kufanikisha hayo serikali yake itaziondoa Tax bubu zote, na utaratibu wa kuweka rangi na namba kwenye magari utarudi ili Tax zote zitambulike.

Aidha amesema madereva wa tax kutoa taarifa za matukio ya kiharifu pale wanapohisi abiria waliyempakia ni mtu wa kufanya matukio ya kialifu.
 Makonda amesema wakitoa taarifa za uhalifu watalisaidia Taifa kuwa katika hali ya usalama, huku akiwataka ndani ya wiki moja wakae wajadiliane waje na mapendekezo yatakayokuwa na tija kwa pande zote.

Makamu Mwenyekiti wa Madereva  mkoa wa Dar es Salaam, Jacob Anyandwile amesema madereva hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutozwa kodi kubwa na Mamlaka ya mapato nchini (TRA) pamoja na uwepo wa huduma ya Tax kwa njia ya mtandao unafanywa na kampuni ya UBA ambayo  imechangia kuharibu  soko ya usafiri huo.
Amesema kampuni ya UBA inatoza bei ndogo zaidi, pia gharama za uendeshaji hazilingani wanajikuta wao wanalipa kodi kubwa zaidi kuliko kampuni hiyo.

Katibu Mkuu wa Umoja huo Ramadhani Ashiru ameeleza kuwa kampuni hiyo ya UBA inatumia Tax bubu ambazo hazitambuliki kisheria.

No comments:

Post a Comment