Tuesday, January 24, 2017

TRL YAREJESHA SAFARI YA TATU AWAMU YA JIONI KWA TRAIN YA DAR_ PUGU KUANZIA JANUARY 25/2017

Na. John Luhende
KamKampuni ya reli Tanzania TRL imesema  safari za train yakwenda Pugu awamu ya jioni zilizo kuwa zimesitishwa zitaanza tena siku ya jumatano January  mwaka huu  na safari Zita anzia kituo kikuu cha Dar es salaam saa2:15 usiku na kuwasili Pugu saa 3:10 usiku.

Akizungumza na waandishi wa habari  kaimu Mkuu wa usafirishaji  na reli Rashidi Ng'wani  amesema kureje kwa safari hizo kuna fuatia kukamilikakwa matengenezo ya kutandika reli mpya katika eneo korofi  kati ya stesheni  za Ilala  block  post na karakata.

Aidha amesema kuwa safari za awamu ya asubuhi zitaendelea kuwa mbili tu  kwa kuwa kazi ya ukarabati haijakamilika baadhi ya maeneo , kazi ya ukarabati wa reli ulianza  January 2/ 2017.

Ameongeza kuwa ukarabati huu unalengo la kuimarisha njia ya reli katika eneo hilo ambalo kwasasa linapitisha train nyingi  kwa siku kuliko ilivyokuwa imezoeleka hapo awali.
Hata hivyo ukara huo  uraondoa kero ya vumbi kwa abiria kwenye mabehewa  kwa kuwa njiayite itawekwa kokoto  za kutisha ambazo hazina vumbi .

Ukarabati huu ni wakubadilisha reli ndogo za ratili 60 na kuweka reli kubwa za ratili 80 ambazo ni imara zaidi na kuwezesha gari Moshi kutembea kwa usalama zaidi.

No comments:

Post a Comment