Kaimu Kamishna Utawala na Fedha kutoka Jeshi la Uhamiaji Bw. Abbas Irovya wa pili kutoka kushoto akiongea na wanahabari hawapo pichani kuhusu ripoti ya operesheni mbalimbali zinazoendelea kufanyika nchini kwa lengo la kudhibiti wahamiaji haramu,wa kwanza kulia ni Mkaguzi wa Uhamiaji Bw. Leslie James Mbotta na wa kwanza kulia ni Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo Bi. Rosemary Mkandala.(Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).
Frank Mvungi-Maelezo.
Takribani raia 4792 wa kigeni wamekamatwa kwa kukiuka sheria, Kanuni na Taratibu za Uhamiaji katika kipindi cha Januari hadi aprili mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salam na Kaimu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abass Irovya wakati wa mkutano na Vyombo vya habari uliolenga kutoa taarifa ya Operesheni mbalimbali zinazotekelezwa na Idara hiyo.
Irovya amesema kuwa Idara hiyo imekuwa ikiendesha Operesheni ondoa uhamiaji haramu tangu mwezi Desemba mwaka jana na imeonyesha mafanikio ambapo raia 1796 wamefukuzwa nchini kwa kukiuka sheria za uhamiaji.“Wananchi walio wengi wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa Idara yetu kutokana na uelewa wao kuongezeka kwa sababu tunayo programu ya kutoa elimu kwa umma na imeonyesha mafanikio makubwa” alisisitiza Irovya
Bw. Irovya aliongeza kuwa waliohukumiwa kifungo ni raia 132 na 383 kesi zao zinaendelea kwenye mahakama katika Mikoa mbalimbali hapa nchini.Raia 388 walilipa faini hali iliyochangia kuongeza mapato ya Serikali kutokana na kukiuka sheria na Kanuni za Uhamiaji hapa nchini.
Kwa upande mwingine kesi 509 zinaendelea katika mahakama mbalimbali hapa nchini na raia 294 waliachiwa huru kutokana na mahakama kutowatia hatiani.Idara ya Uhamiaji ina Vituo takribani 60 katika Mikoa Mbalimbali hapa nchini baadhi vikiwa katika Mikoa ya anga,Lindi,Mtwara,Ruvuma,Katavi,Kigoma,Simiyu ambapo Idara hiyo imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari za raia wa kigeni wanaoingia nchini bila kufuata sheria na taratibu za Uhamiaji.
No comments:
Post a Comment