Tuesday, June 14, 2016

MANISPAA YA ILALA KUKUSANYA MAPATO KWA KUTUMIA KIKOSI KAZI.

 Mkurugenzi wa Manispaa  ya Ilala, Isaya Mngurumi akizungumza na wandishi wa habari juu ya hatua zilizochukuliwa na Manispa hiyo kwa wadaiwa Sugu wa mapato na ushuru mbalimbali, (Kulia) ni Meya wa Manispaa hiyo Charles Kuyeko na Naibu Meya , Omary Kambilamoto.
Naibu Meya , Omary Kambilamoto Akishusha mabango yaliyowekwa bila kulipa ushuru.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala imeunda kikosi kazi maalum cha kukusanya mapato ili kuweza kufikia malengo waliyojipangia ya Sh. Bilioni 55.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mungurumi amesema kikosi hicho kimeweza kukusanya sh.bilioni moja kwa wiki huku ikiwa lengo ya kukusamya sh.bilioni 15 kwa mwezi mmoja.

Amesema kuwa katika ukusanyaji wa mapato hayo wamebaini kuwepo kwa watu wenye leseni feki za biashara pamoja na vibali feki vya ujenzi wa maghorofa katika manispaa ya Ilala.
Mungurumi amesema kuwa watu wamejenga maghorofa bila   kuwa na  sehemu ya  kuegesha magari  ambapo ni kosa na kutakiwa wote waliofanya hivyo kujisalimisha.

Aidha amesema kuwa wataendelea kupambana watu wanaokwepa kodi za manispaa ambazo ndizo zinazofanya kuboresha huduma kwa wananchi ya kuweza kupata maji safi na salama, upatikanaji wa madawati pamoja na ujenzi wa miundombinu mbalimbali.

Naye Meya wa Manispaa hiyo, Charles Kuyeko amesema kuwa manispaa inafatilia vyanzo vyote vya mapato ili kuweza kufikia malengo yao.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Isaya Mungurumi akizungumza na waandishi wa habari juu kikosi kazi cha ukusanyaji mapato katika manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam,

No comments:

Post a Comment