Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja, akimkaribisha Spika mstaafu wa Bunge Mhe. Anna Makinda pale kiongozi huyo alipotembelea taasisi hiyo kwa mara yake ya kwanza.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja akimuelezea Spika mstaafu Mhe. Anna Makinda kuhusu mpango wa ujenzi wa ofisi za kudumu za Taasisi hiyo zilizopo katika kijiji cha Kondo, wilayani Bagamoyo.
Spika mstaafu Mhe. Anna Makinda akiweka saini yake katika kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika ofisi za Taasisi ya Uongozi zilizopo Oyster Bay jijini Dar es Salaam mapema leo.
Spika mstaafu Mhe. Anna Makinda akimuonesha Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja kitabu cha muongozo na kanuni za Bunge.
Mazungumzo yakiendelea kati ya Spika mstaafu Mhe. Anna Makinda na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja.
No comments:
Post a Comment