Tuesday, June 14, 2016

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI MHE. MWIGULU NCHEMBA NA MHE. CHARLES TIZEBA

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli  Ikulu Jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Juni, 2016 amewaapisha mawaziri wawili kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri aliyoyafanya Jumamosi tarehe 11 Juni, 2016.

Mawaziri walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es salaam ni Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba aliyeapishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi anakwenda Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, akitokea Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.Waziri mwingine ni Dkt. Charles John Tizeba ambaye ameapishwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Dkt. Charles John Tizeba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Buchosa aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuanzia tarehe 11 Juni, 2016.

Hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
13 Juni, 2016 . 

No comments:

Post a Comment