Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza na wananchi wa kijiji cha mwavi kata ta Fukayosi Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani katika mkutano maalumu na kutatua sakata la mgogoro wa ardhi baina yao pamoja na mwekezaji Mkorea, ambaye amepokonywa hekari 131 na zimerudishwa kwa wananchi wenyewe.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Baadhi ya wawekezaji hao ambao ni wakorea wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika mkutano huo.
SAKATA la mgogoro wa ardhi kwa wananchi wa kijiji cha mwavi kata ya Fukayosi kilichopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na mwekezaji ambaye ni mkorea limechukua sura mpya baada ya mkuu wa Wilaya hiyo kuamua kuliingilia kati suala hilo kwa lego la kurudisha hali ya amani na utulivu pamoja na kumaliza tofauti zilizokuwepo.
Mgogoro huo ambao umeonekana kuwa na mvutano mkubwa kutokana na mwekezaji huyo kupatiwa eneo lenye ukumbwa wa hekari 231 za serikali ya kijiji pasipo kuwashirikisha wananchi wenyewe kitu ambacho kilichangia kwa kiasi kikubwa kutoelewana kati ya wanakijiji na mwekezaji huyo.
Akizungumzia kuhusina na sakata hilo Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga alisema kwamba baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao aliamua kufanya uchunguzi wa kina na kubaini mwekezaji huyo alipewa eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji,ambapo kwa sasa wamekubaliana naye hekari 131 zirudishwe kwa wananchi wenyewe na yeye abakiwe na hekari 100 tu.
“Jamani wananchi wa kijiji cha mwavi mimi baada ya kuniletea malalamiko hayo nimeyafanyia kazi kwa kina kabisa ambapo nimekutana na mwekezaji huyo tumeongea naye juu ya suala hilo na amekubali kuzirudisha hekari 131za ardhi kwa wananchi nayeye atabakiwa na hekari 100 kwa ajili uwekezaji katika eneo hilo ambapo atajenga kituo cha kilimo, shule, zahanati pamoja na mambo mengine hivyo tuwe watulivu tumwone kama ataziendeleza kama tulivyokubaliana.
No comments:
Post a Comment