Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo akimkabidhi kadi ya uanachama Goodluck Ole Medeye aliyekuwa mwanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwenye Makao Makuu ya Chama hicho Mwananyamala Kinondoni jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo akimshuhudia Bw. Goodluck Ole Medeye wakati akionyesha kadi ya uanachama aliyokabidhiwa baada ya kujiunga na Chama cha UDP akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA leo kwenye Makao Makuu ya Chama hicho Mwananyamala Kinondoni jijini Dar es salaam.
wenyekiti wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo akimpongeza mke wa Goodluck Joseph Ole Medeye mara baada ya mume wake kujiunga na Chama cha UDP .
Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, aliyedumu na chama hicho kwa miezi kumi na moja Goodluck Ole Medeye, amekihama chama hicho na kujiunga na United Democratic Party UDP.
Bw. Medeye aliyewahi kuwa Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na kuitumikia serikali katika nafasi ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ametangaza uamuzi wa kuhama Chadema jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa kadi ya UDP na Mwenyekiti wa Chama hicho John Momose Cheyo.
Mbunge huyo wa zamani wa jimbo la Arumeru Magharibi amejiunga na UDP akiwa na Mkewe, pamoja na watu wengine tisa wakiwemo waliokuwa kwenye vyama tofauti na wengine waliodai hawakuwahi kuwa kwenye siasa, ambapo katika maelezo yake, Ole Medeye amesema awali alitaka kuunda chama kipya lakini baada ya kupitia katiba za vyama akaona UDP ni sehemu sahihi.
Kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini, wanasiasa hao wamelaani uminywaji wa demokrasia katika kipindi hiki, hususan ndani ya Bunge, na kushauri wabunge wa kambi ya upinzani wanaosusia vikao kurejea ndani ya ukumbi wa Bunge kwa vile njia wanayotumia haitabadili utaratibu wa kibunge hususan kumuondoa Naibu Spika kwenye kiti chake.
No comments:
Post a Comment