Wednesday, June 22, 2016

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA OFISINI HAZINA

 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango,  Bw. Gideon Manambo akiongea na watumishi wa wizara. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Doto James.
 Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano wa pamoja
 Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifanya sala wakati wa kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano wa pamoja
 Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati wakiadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano wa pamoja
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati wakiadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano wa pamoja. Hapa baadhi yao wakiwa katika picha ya pamoja.

Wizara ya Fedha na Mipango imeadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano na Watumishi wake, lengo likiwa ni kujadili mafanikio na changamoto wanazo kabiliana nazo mahali pa kazi. 

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Doto James aliwataka Watumishi kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. John Magufuli katika  kupambana na masuala ya rushwa, uzembe kazini na Watumishi hewa ambao wamekuwa wakiigharimu Serikali fedha nyingi katika kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Alisema Wizara inajipanga kuhakikisha inaboresha mazingira ya kazi kwa watumishi hasa kwa wale wenye ulemavu kwa  kuwajengea miundombinu rafiki sehemu za kazi ili  kuongeza ufanisi kazini.

"Wizara pia inafanya vizuri katika masuala ya usawa wa kijinsia kwa kuwa na idadi inayoridhisha ya wanawake hasa katika ngazi za maamuzi, ikiwa ni pamoja na kuwa na Manaibu Katibu Wakuu wawili wanawake" . Alisisitiza James

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango,  Bw. Gideon Manambo alisema kuwa, watumishi wanatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi na kwa  bidii ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya maendeleo ambayo yanahitaji watendaji wenye weledi wa kutosha ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.

Kwa upande wa watumishi wa Wizara, wameuomba uongozi kuhakikisha kunakuwepo na vitendea kazi vya kutosha ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa na matokeo chanya ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayowakabili wananchi.

Maadhimisho hayo yamefanyika kufuatia utaratibu mpya uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano ambapo uliagiza Wizara pamoja na Taasisi kuadhimisha Wiki hiyo kwa kutatua matatizo ya watumishi wa Umma pamoja na wananchi kwa ujumla katika maeneo yao ya kazi.

Imetolewa na:
B. Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

No comments:

Post a Comment