Monday, June 06, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA IBADA KANISA LA MAOMBEZI LA MCHUNGAJI ANTONY LUSEKELO ‘MZEE WA UPAKO’ UBUNGO KIBANGU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ katika kanisa lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na kukagua barabara inayotoka Ubungo Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo la Riverside.
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Anthony Lusekelo ‘mzee wa upako akiagana na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuhudhuria  ibada katika Kanisa la Maombezi Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Dkt. Magufuli akiwashukuru waumini (hawapo pichani ) wa kanisa hilo la Maombezi la Mzee wa Upako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakitoka kwenye kanisa la Maombezi la Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment