Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni Dar es Salaam Bw Achiles Bufure, akifafanua jambo kwenye Mkututano na
wasanii wa Kimataifa wa Ngoma za Ubunifu na Muziki, awapo pichani.
Msanii wa Kimataifa wa Ngoma za Ubunifu Bw
Aloyce Makonde akifafanua jambo kwenye Mkututano na Uongozi wa
Makumbushona Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Msanii wa Kimataifa wa Ngoma za Ubunifu na
Muziki wa asili Bw Isack Abeneko akifafanua jambo kwenye Mkututano na Uongozi
wa MakumbushonaNyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni Dar es Salaam Bw Achiles Bufure, pamoja na wajumbe wa kikao
wakisikiliza kwa makini ufafanuzi kutoka kwa Msanii wa Kimataifa wa ngoma za
Ubunifu na Muziki Bw Isack Abeneko (walipi kushoto) kwenye Mkutano maalum wa
maandalizi ya Onesho la sanaa litakalofanyika Tar 24 June 2016 kwenye Ukumbi wa Makumbusho Posta mjini Dar
es Salaam.
Na Sixmund J. Begashe
Makumbusho
na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, imefungua mlangoa kwa wasanii wa ndani ya
nchi na marachache wa kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuwapa nafasi wasanii wa
wakitanzania kuibua na kuendeleza vipaji vyao kwa kufanya maonesho ya mara kwa
mara katika kumbi za maonesho zilizopo katika Makumbusho hiyo.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure
kwenye mazungumzo na muandishi wa habari hizi baada ya kikao walicho kaa na
wasanii wa Ngoma za Ubunifu ambao hufanya kazi zao kimataifa na marachache
ndani ya nchi .
Bw,
Bufure alisema kuwa kwa sasa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni imeanzisha
Progaram Maalumu inayoitwa MUSEUM ARTS EXPLOSION ambapo kila mwisho wa mwezi
wasanii watapata nafasi ya kufanya Maonesho kwenye Ukumbi wa kisasa wa
Makumbusho hiyo na kwa mwezi huu wa Juni Wasanii wa Kimataifa Bw Aloyce Makonde
na Bw Isack Abeneko pamoja na wasanii
wengine watafanya onesho kubwa siku ya tare 24 jioni.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti Bw Aloyce Makonde na Bw Isack Abeneko wameitaja program iliyo
anzishwa na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kuwa ni ya kizalendo na
itarudisha heshma ya kazi za sanaa na wasanii kwenye fikra za watanzania na
ulimwengu kwa ujumla.
‘’Naipongeza
sana Makumbusho ya Taifa kwa kuanzisha program hii, kwa sababu kilikuwa ni
kilio cha muda mrefu cha wadau wa sanaa na wasanii nchi kutokuwa na sehemu
yenye heshma zaidi itakayoweza kuwakutanisha wasanii na wapenzi wa sanaa zenye
asili ya utamaduni wa kitanzania, lakini kilio hicho kimefutwa machozi na
serikali kupitia Makumbusho ya Taifa na ninaomba program hii iwe endelevu”
Alisema Bw Makonde.
Nae
Bw, Abeneko aliongeza kuwa ni wakati sasa kwa watanzania kuona sanaa zenye
ubora zaidi kupitia ukumbi wa Kisasa wa makumbusho hiyo kwani niimani yake kuwa
wasanii wote watajiandaa vya kutosha kabla ya kupandisha kazi zao kwenye stage
hiyo ya kisasa hapa nchini. “Hivi juzi mimi nilikuwa Ujerumani kwa maonesho ya
takribani mwezi mzima, nimeona namna sanaa yenye vionjo vya utamaduni wetu
inavyo pendwa na kuheshimiwa huko nje, naamini kwa mlango huu sasa watanzania
nao watapata nafasi ya kuidhamini” aliongeza Bw Abeneko.
Bw.
Bufure ametoa wito kwa wasanii na watanzania wote kujitokeza siku ya Tarehe 24
June saa moja jioni kushuhudia onesho hilo la Contemporary Dance litakalofanywa
na DANCE GARGE chini ya Msanii Aloyce Makonde na Isack Abeneko, kama onesho la
ufunguzi wa program hiyo ambapo kiingilio kitakuwa ni Tsh 10,000/= (elfu kumi)
kwa wakubwa na wanafunzi Ths 5000 (elfu tano)
No comments:
Post a Comment