Wednesday, June 22, 2016

RAIS MAGUFULI AZINDUA SARAFU YA KUMBUKUMBU YA SHILINGUI ELFU HAMSINI JIJINI DAR ES SALAAM:


[​IMG]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 22, 2016
[​IMG]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisimama kwa ukakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa akiwa na katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Dkt Servacius Likwelile, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu, na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam
[​IMG]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam
[​IMG]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizindua sarafu maalumu ya shilingi 50,000/- kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania
[​IMG]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na Magavana na Manaibu Magavana na menejimenti ya BOT kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania.
Rais Magufuli katika hotuba yake kwenye maadhimisho haya ambayo yamehuduriwa na Magavana na Naibu Magavana wa Benki Kuu, Rais Magufuli pia amesema baadhi ya changamoto ambazo zinaikabili Benki Kuu ni usimamizi wa huduma za kifedha ili kuwafikia watanzania hadi vijijini.

Aidha Rais Magufuli amesema Benki Kuu inatakiwa kudhibiti matumizi ya dola ili kulinda thamani ya shilingi, kulinda ubora na usalama wa matumizi ya kielekroniki pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei.

Wakati huo huo Rais Magufuli amesema uamuzi wa serikali kusitisha ajira mpya pamoja na kupandisha vyeo watumishi wa serikali ni wa muda mfupi ili kudhibiti tatizo la watumishi hewa

Awali akielezea historia ya Benki Kuu tangu kuanzishwa kwake June 14 mwaka 1966, Gavana Beno Ndulu amesema Benki Kuu imeweza kujiendesha yenyewe bila ya kutegemea serikali.

Katika maadhimisho hayo Rais Magufuli pia amezindua Sarafu ya Shilingi Elfu hamsini kwa ajili ya kumbukumbu pamoja na kupokea Hundi ya Shilingi Bilioni nne ikiwa ni mchango wa ajili ya madawati.

Magavana na Naibu Magavana kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa wamehudhuria maadhimisho haya.

No comments:

Post a Comment